Hivos Yaipongeza ShujaazFM
Mojawapo wa mashirika wafadhili wa Twaweza, Hivos, limepongeza mradi wa ShujaazFM kwa kupokea Tuzo ya OneWorld ya Vyombo Habari Mahsusi kwa jinsi inavyowafikia mamilioni ya vijana nchini Kenya.ShujaazFM ambao ni mbia wa Twaweza hugawa nakala 600,000 za kitabu cha vikaragosi, hutangaza kila siku redioni, hufanya mijadala ya mitandao na kutuma jumbe za simu za mkononi kuwatia moyo na shime vijana wa Kenya wachukue hatua kuboresha maisha yao kwa kujihusisha na masuala halisi yanayohusu mustakabali wao. Makala hiyo pia itakuunganisha na mahojiano na Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Bwn. Alan Duncan, ambaye anaipongeza kazi ya ShujaazFM kwenye tafrija ya kutoa zawadi za OneWorld Media jijini London mapema mwaka huu. Soma zaidi.
Endelea kusoma: agency shujaazFM vijana wabia wa elimu wadau wa Twaweza Kenya zawadi
unaweza pia kupenda...
- ShujaazFM yashinda tuzo Maalumu ya One World Media (20 May 2011)
- Zabuni za kuendesha taftishi wananchi kwa simu ya mkononi inatangazwa (20 Jan 2012)
- Nafasi mpya za kazi zinapatikana Tanzania, Kenya na Uganda! (21 Dec 2011)
- Wekeni bajeti wazi wa umma, Serikali zaambiwa (21 Nov 2011)
- Sasa ShujaazFM ipo YouTube (21 Nov 2011)
- Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi Waanza Kazi Afrika Mashariki (25 Oct 2011)
- Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi (15 Sep 2011)

