Matokeo yakipuuzwa, ukaguzi wa nini?
Uwazi, iliyopo Twaweza imetoa muhtasari mpya wa sera unaoitwa, “Matokeo yakipuuzwa, ukaguzi wa nini?” Muhtasari huu unatumia ripoti za ukaguzi wa hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutathmini mabadiliko katika ubora wa usimamizi wa fedha katika Mamlaka hizo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Tathmini inaonesha kwamba viwango vya ubora wa hati za ukaguzi havikupanda na kwamba hata baada ya miaka mitano ya ukaguzi, usimamizi wa fedha katika Mamlaka nyingi za Serikali za Mitaa bado ni dhaifu. Kwa kiasi kikubwa mapendekezo kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali yanapuuzwa, na hata hoja za ukaguzi hazifanyiwi kazi.
Muhtasari huu unapendekeza kwamba Tanzania iweke vichocheo vitakavyohakikisha kwamba mapendekezo yanayotokana na ukaguzi yanafanyiwa kazi. Mamlaka inayoteua timu za menejiment za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wabunge, Kamat za Uwajibikaji za Bunge, na Wajumbe wa Halmashauri wana wajibu mkubwa kat ka kuhakikisha kwamba jambo hili linafanikiwa. Soma muhtasari mzima.
Endelea kusoma: machapisho ukaguzi Uwazi
Authors: Uwazi
Organizations: Uwazi
unaweza pia kupenda...
- Shule za msingi za Serikali Dar es Salaam:Vyoo vibovu, michezo kidogo. (2 Jun 2011)
- Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam:Msongamano wa wanafunzi bila vitabu vya kiada vya kutosha (2 Jun 2011)
- Wabunge waongeaji Bungeni ndio hutetea viti vyao tena? (14 Apr 2011)
- Dar es Salaam wanachukuliaje utawala? (19 Dec 2012)
- Wakazi wa Dar wanasemaji kuhusu afya? (18 Sep 2012)
- Je Watoto Wetu Wanajifunza? Kuhesabu na Kusoma Katika Afrika Mashariki (28 Jul 2011)
- Boresho la "Je, wanafanya kazi kwa ajili yetu?" (24 Jun 2010)

