Twaweza.org

Mwanzo

Twaweza ni nini?

Twaweza ni kusema kwamba tunaweza kufanya mambo yakawa. Hii ni jitihada mpya inayomlenga raia na inayokusudia kuleta mabadiliko makubwa Afrika Mashariki. Twaweza inaamaini kwamba mabadiliko ya kudumu hayana budi kuanzia chini kwenda juu. Tumedhamiria kujenga mazingira na kupanua fursa ambazo zitatoa mwanya kwa mamilioni ya watu kuhabarishwa and kuwawezesha kuweza kuleta maendeleo katika jamii zao moja kwa moja na kuifanya serikali iwajibike. Soma zaidi.

Ufafanuzi kuhusu Matokeo ya Kidato cha Nne

Kwa wiki kadhaa, Twaweza na Mkuu wa shirika letu, Rakesh Rajani, tumepokea maombi mengi ya kutaka ufafanuzi kuhusiana na Matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne 2012, na juu ya uamuzi wa Serikali kupanga upya matokeo hayo. Endelea kusoma...

Wananchi Wazungumza kuhusu Matokeo ya Kidato cha Nne

Wazazi wana ufahamu kuhusu mwendelezo wa kuanguka kwa ubora wa elimu ya sekondari, na kwa kiasi kikubwa wanatupa lawama kwa serikali na walimu kwa kuanguka huko.Matokeo haya yamechapishwa katika muhtasari wa Twaweza unaoitwa Matokeo ya Mtihani wa Kid... Endelea kusoma...

Sauti za Wananchi

Uwazi iliyopo Twaweza imezindua utafiti wa awali wa Sauti za Wananchi (Voices of Citizens), ambao ni mradi mpya unaotumia simu za mkononi ili kukusanya taarifa za mara kwa mara kutoka katika wigo mpana wa wananchi wa Tanzania. Mradi huu utawezesha da... Endelea kusoma...

Mpango wa KiuFunza - Kiu ya Kujifunza - Wazinduliwa

Mpango mpya wa utekelezaji wa sera za Elimu, inayojulikana kama KiuFunza, itakayojaribu kutekeleza utaratibu wa kupeleka kiasi kamili cha ruzuku kwa kila mwanafunzi moja kwa moja shuleni kwa ajili ya uendeshaji wa shule; na kuwalipa walimu motisha kw... Endelea kusoma...

Dar es Salaam wanachukuliaje utawala?

Wakazi wa Dar es Salaam hawaridhishwi na hali ya utoaji wa huduma, hawana imani na taasisi za umma na hawazielewi vizuri sera. Wapo walioripoti kuchukua hatua ili kubadili hali zao. Endelea kusoma...

Machapisho

Iliyovutia


  • Shindano! Kila robo ya miaka 2013 - kompyuta ndogo (laptops) ishirini zitatolewa kwa washindi na kwa shule watakazozichagua. Toa maoni yako kuhusiana na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii kushinda kabla ya tarehe 1 Novemba 2013. Endelea kusoma...




  • Twaweza imeanzisha kitengo cha Uwazi ambacho kinawapa wabia wa Twaweza, vyombo vya habari na mawakala wakuu wa mabadiliko (wabunge, waandishi wa habari, wakuu wa serikali) taarifa zilizojengwa juu ya msingi wa takwimu, na zinazowasilisha ujumbe ulio ... Endelea kusoma...