Ripoti mpya ya Uwezo yapiga mbiu Afrika Mashariki
15 Jul 2011
hot
|
Matangazo
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu amewapa changamoto wadau wa elimu kuboresha kiwango cha elimu ya msingi kwa nchi za Afrika Mashariki iwapo Jumuiya hiyo inataka kushindana kimataifa. Balozi Mwapachu amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye hotuba ya kuzindua ripoti ya elimu kwa nchi za Afrika Mashariki. Ripoti hiyo mpya inaonesha kuwa wanafunzi wa madarasa ya juu ya elimu ya msingi nchini Kenya, Uganda na Tanzania walishinda kufauli majaribio ya darasa la pili.
“Jumuiya hii itayumba katika mipango na matarajio ya malengo yake iwapo kiwango chake cha elimu ya msingi kitabakia hivi kilivyo leo,” amesema Balozi Mwapachu. Unaweza kusoma hotuba yake nzima ukibofya hapa. Fungua ripoti kwenye sehemu ya machapisho.
Endelea kusoma: elimu Afrika Mashariki Hotuba ya Juma Mwapachu Uwezo
unaweza pia kupenda...
- Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi (15 Sep 2011)
- Ripoti ya Serikali ya Uganda Inaakisi ya Uwezo (15 Jul 2011)
- Tuboreshe viwango vya elimu ya msingi, si idadi (15 Jul 2011)
- Uwezo Kenya kuzindua ripoti ya upimaji ya mwaka 2011 (20 Jun 2011)
- Uwezo yatambuliwa magazeti ya Tanzania, Guardian la Uingereza, na katika Mkakati Mpya wa Benki ya Dunia kwa Afrika (18 Mar 2011)
- Kipeperushi-Je Watoto wetu wanajifunza? (1 Nov 2010)
- Wanafunzi wengi hawajui kusoma, kuandika-Utafiti (23 Sep 2010)