Twaweza.org

Sauti za Wananchi

    
To read this in English, go here.

Uwazi iliyopo Twaweza imezindua utafiti wa awali wa Sauti za Wananchi (Voices of Citizens), ambao ni mradi mpya unaotumia simu za mkononi ili kukusanya taarifa za mara kwa mara kutoka katika wigo mpana wa wananchi wa Tanzania. Mradi huu utawezesha data za awali/msingi kukusanywa kwa haraka na kwa ufanisi, kwa gharama ya chini, kuwataarifu wananchi kuhusu yale yanayoendelea na kuwasaidia watunga sera kushughulikia kwa ukaribu zaidi mahitaji na matamanio ya raia. Zaidi

< iliyopita 123...121314
40 makala
Sort by: Maoni |

Tanzania: Afya Kwanza

Wananchi wanapopata majeraha ama kuugua, 6 kati ya 10 (61%) huenda katika kituo cha afya cha serikali. Kiwango hiki kimeongezeka kutoka 45% mwaka 2014 na kubaki hivyo hivyo tangu mwaka 2016. Kwa kiasi kikubwa hii imesababishwa na kupungua kwa watu wanaojitibu wenyewe kwa kwenda kwenye maduka ya dawa (9%), maduka ya kawaida kupata dawa (7%), wasiofanya chochote (1%) au wanaotafuta aina nyingine za matibabu (5%). Takwimu zilizokusanywa toka mwaka 2014 zinaonesha kupungua kwa matumizi ya njia hizo. Idadi ya wananchi wanaotumia vituo binafsi, vya kanisa ama vya mashirika yasiyo ya kiserikali haijabadilika katika kipindi hiki (16% mwaka 2017).

Hapa Usalama Tu

Kuna mtazamo wa jumla miongoni mwa wananchi kuwa usalama nchini umeimarika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kama inavyooneshwa na zaidi ya nusu ya wananchi hao (asilimia 53).

Matarajio na matokeo

Muhtasari huu umebeba maoni ya wananchi juu ya masuala ya kisiasa. Kwa mtazamo wao, ni tati zo gani kuu linaloikabili nchi kwa sasa? Je, tati zo hilo limebadilika ukilinganisha na miaka iliyopita? Je, wananchi wanauonaje utendaji wa viongozi wao, akiwemo Rais? Na je, kuna mabadiliko yoyote kati ka kukubalika kwa vyama mbalimbali vya siasa kati ka kipindi cha miaka michache iliyopita?
< iliyopita 123...121314
40 makala
Sort by: Maoni |

Sehemu