TEDxDar na mikinzamo ya maendeleo
TEDxDar, iliyoandaliwa na kundi la vijana wa Kitanzania mwishoni mwa mwezi Mei, ni tukio la kujitegemea limelozaliwa na TED, “jamii” ya kimataifa iliyojikusanya kinamna fulani ikiunganishwa na “fikra zinazostahili kusambazwa kwa teknolojia, burudani na sanaa au ubunifu”. Tukio hili liliweza kuwakutanisha wavumbuzi wa kusisimua ndani ya Tanzania. Kiongozi wa Twaweza, Rakesh Rajani, alizungumzia wapi vuguvugu la mabadiliko linapoanzia, akiibua mifano toka katika uzoefu wake wakati wa uchambuzi yakinifu (wa kitafiti) wa hali ilivyo wakati wa uundwaji wa Twaweza, pamoja na ziara ya mafunzo vijijini iliyofanywa na wafanyakazi wa Twaweza mwaka 2009. Ziara hii imekua ikijadiliwa kwa mapana katika majukwaa ya blogu mbalimbali kwa wiki kadhaa zilizopita, zikipeperushwana Owen Barder, Swahili Street, Elsie Eyakuze na wengineo. Unaweza kufatilia haya majadiliano na pia soma kuhusu uzoefu wa Twaweza katika vijiji tisa ndani ya Tanzania.
Endelea kusoma: Rakesh Rajani TEDxDAR
pakua nyaraka
- Simulizi za Vijiji Tisa | 2.88 MB
unaweza pia kupenda...
- Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi Waanza Kazi Afrika Mashariki (25 Oct 2011)
- 'Kuukomboa wakati' (24 Jun 2010)
- Zabuni za kuendesha taftishi wananchi kwa simu ya mkononi inatangazwa (20 Jan 2012)
- Nafasi mpya za kazi zinapatikana Tanzania, Kenya na Uganda! (21 Dec 2011)
- Wekeni bajeti wazi wa umma, Serikali zaambiwa (21 Nov 2011)
- Sasa ShujaazFM ipo YouTube (21 Nov 2011)
- Vyombo vya habari Afrika Mashariki vyaandika kuhusu Ushirikiano wa Serikali Zilizo Uwazi (13 Oct 2011)

