Twaweza.org

Ufuatiliaji wa Mahudhurio ya Shule Uganda

Twaweza inashirikiana na SNV Uganda katika mradi wa majaribio kuhusu kujifunza nchini Uganda kwa lengo la kufuatilia mahudhurio na utoro wa walimu na wanafunzi katika shule za msingi kwa kutumia ujumbe mfupi (sms), lengo likiwa ni hatimaye kuusambaza ufuatiliaji huu katika nchi nzima (shule za msingi 16,000). Viwango vya utoro wa walimu mashuleni nchini Uganda vinakadiriwa kuwa kati ya 20% na 30%, ambavyo ni miongoni mwa viwango vikubwa zaidi duniani, na athari zake kwa elimu ni dhahiri. Mradi huu utaanza kwa majiribio katika wilaya mbili kwa kutumia nyenzo ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kufuatilia mienendo ya mahudhurio ya walimu na wanafunzi katika shule za msingi 100. Taarifa hizi zitaonyesha kwa uwazi kuhusu utoro wa walimu na wanafunzi na zitawasaidia maafisa wa serikali katika ngazi za wilaya na chini yake kuchukua hatua zainazopasa za muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, na kuwawezesha pia wadau wasio wa kiserikali kuchukua hatua  zifaazo dhidi ya tatizo hili. Taarifa hizi zitatolewa kwa wadau mbali mbali katika jumuiya za shule ili kuhamasisha uchukuaji wa hatua kuibadilisha hali hii. Matumaini ni kwamba mahudhurio ya walimu na wanafunzi yataboreshwa kutokana na upatikanaji wa takwimu halisi za hali ilivyo.

Endelea kusoma: Elimu Uganda ubia utoro wa waalimu

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri