Uwezo Kenya kuzindua ripoti ya upimaji ya mwaka 2011
Taasisi ya wanawake watafiti wa elimu Kenya imetangaza kuwa mnamo Julai 19 mwaka huu itazindua ripoti ya upimaji wa Uwezo kitaifa ya mwaka 2011. Wakati uzinduzi wa ripoti hiyo ukifanyika kitaifa kwenye viwanja vya Taasisi ya Elimu ya Kenya (KIE) kutakuwa pia na matukio ya uzinduzi kwenye mikoa ifuatayo: Magharibi, Bonde la Ufa, Mashariki, Kaskazini Mashariki na Eldoret. Lengo la maadhimisho ya kimkoa ni kuwahusisha wadau wengi zaidi wa elimu wakati wa kutoa matokeo ya utafiti na hivyo kuwahamasisha raia kuchukua hatua kuboresha kiwango cha elimu inayotolewa mashuleni.
Njoo mara nyingine kwenye tovuti hii usome habari zaidi za uzinduzi huo.
Endelea kusoma: kenyan primary education Uwezo Uwezo assessment report launch 2011 Uwezo Kenya
unaweza pia kupenda...
- Uwezo yaunga mkono mabadiliko katika mfumo wa elimu nchini Kenya (10 Feb 2012)
- Ripoti ya Uwezo 2011 yatoa mwangwi kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki (13 Oct 2011)
- Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi (15 Sep 2011)
- Ripoti mpya ya Uwezo yapiga mbiu Afrika Mashariki (15 Jul 2011)
- Uwezo yatambuliwa magazeti ya Tanzania, Guardian la Uingereza, na katika Mkakati Mpya wa Benki ya Dunia kwa Afrika (18 Mar 2011)
- Kipeperushi-Je Watoto wetu wanajifunza? (1 Nov 2010)
- Wanafunzi wengi hawajui kusoma, kuandika-Utafiti (23 Sep 2010)

