Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi
Mwaka uliopita, Uwezo ilifanya utafiti nchi nzima kupata picha halisi ya namna watoto wetu wanavyojifunza katika ngazi ya elimu ya msingi. Zaidi ya watoto 40,000 kutoka kaya 20,000 na wilaya 38 za Tanzania Bara walishiriki kwenye zoezi hilo. Huu ulikuwa ni utafiti mkubwa na wa aina yake nchini. Mwaka mmoja baadae… Nini kimebadilika? Je watoto wetu wanajifunza zaidi?
Kwa mwaka huu wa 2011, Uwezo Tanzania imepanua wigo wake wa kiutafiti kwa kuwapima watoto 128,005 kutoka kaya 76,796 ndani ya wilaya 132. Kigezo kilichotumika ni kilekile ambacho ni kuwapima maelfu ya watoto kwa kutumia majaribio ya ngazi ya Darasa la 2. Unaweza kusoma taarifa hiyo ya kitafiti hapa.
Endelea kusoma: Elimu Tanzania Upimaji wa Kujifunza Tanzania 2011 Uwezo
Organizations: Uwezo
unaweza pia kupenda...
- Ripoti mpya ya Uwezo yapiga mbiu Afrika Mashariki (15 Jul 2011)
- Uwezo Kenya kuzindua ripoti ya upimaji ya mwaka 2011 (20 Jun 2011)
- Uwezo yatambuliwa magazeti ya Tanzania, Guardian la Uingereza, na katika Mkakati Mpya wa Benki ya Dunia kwa Afrika (18 Mar 2011)
- Kipeperushi-Je Watoto wetu wanajifunza? (1 Nov 2010)
- Wahitimu darasa la 7 hawajui kusoma (25 Sep 2010)
- Utafiti: Hatima ya elimu yetu hatarini (25 Sep 2010)
- Wanafunzi wengi hawajui kusoma, kuandika-Utafiti (23 Sep 2010)

