Uwezo yaunga mkono mabadiliko katika mfumo wa elimu nchini Kenya
10 Feb 2012
hot
|
Katika vyombo vya habari
Mratibu wa Uwezo nchini Kenya, Dr. John Mugo anaunga mkono mabadiliko yaliyopendekezwa tume iliyoteuliwa na Serikali kwenye mfumo wa elimu nchini Kenya, limeripoti gazeti la Daily Nation. Tume hiyo ya wajumbe 35 imeshauri kuwa Serikali iondokane na mfumo wa 8-8-4 (miaka minane ya elimu ya msingi, minne ya sekondari na minne ya chuo kikuu), ulitekelezwa tangu 1985,na badala yake kuweka mfumo wa 2-6-6-3 ( miaka miwili ya elimu ya awali, sita ya elimu ya msingi, sita ya elimu ya sekondari mitatu ya chuo kikuu)
Mugo anasema mfumo unaopendekezwa utakuwa bora kwa wanafunzi, kwa kuwa msisitizo utakuwa si kufaulu madarasa bali ni kupata stadi zinazotakiwa. Pia wanafunzi watapata mapema mwelekeo wa kazi gani wangependa kufanya baadaye maishani. Mugo alikuwa akiongea katika uzinduzi wa ripoti ya mwaka ya ujifunzaji mapema wiki hii. Soma zaidi.
Endelea kusoma: elimu Kenya Uwezo Uwezo Kenya
unaweza pia kupenda...
- Changieni mawazo mjadala wa elimu, Uwezo Kenya yasema (14 Feb 2012)
- Ripoti ya Uwezo 2011 yatoa mwangwi kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki (13 Oct 2011)
- Uwezo Kenya kuzindua ripoti ya upimaji ya mwaka 2011 (20 Jun 2011)
- Aibu ya shilingi 6 bilioni (15 Feb 2012)
- Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi (15 Sep 2011)
- Ripoti ya Serikali ya Uganda Inaakisi ya Uwezo (15 Jul 2011)
- Tuboreshe viwango vya elimu ya msingi, si idadi (15 Jul 2011)

