Je, watoto wetu wanajifunza?
Kama mzazi utajisikiaje unapogundua mtoto wako wa darasa la saba hawezi kusoma Kiswahili cha darasa la pili? Utapokeaje taarifa hii kuwa nusu ya watoto wanaomaliza shule ya msingi hawawezi kusoma kwa kiingereza hata kidogo? Ung’amuzi huu na mabainisho muhimu yaliwasilishwa na Uwezo Tanzania katika utafiti wao wa ‘Uwezo wa watoto kusoma na kuhesabu Tanzania 2010. Uzinduzi wa ripoti hii ulifanyika tarehe 21 Septemba, 2010. Utafiti huu ulipima ustadi wa kusoma na kuhesabu kwa zaidi ya watoto 40,000 kutoka kaya 20,000—ukiwa utafiti mkubwa wa aina yake. Matokeo muhimu na mapendekezo ya msingi ya ripoti hii yanaweza kupakuliwa hapa chini:
Endelea kusoma: kuandika kujifunza kusoma Tanzania Uwezo
pakua nyaraka
unaweza pia kupenda...
- Wahitimu darasa la saba hawajui kusoma hadithi (25 Sep 2010)
- Kipeperushi-Je Watoto wetu wanajifunza? (1 Nov 2010)
- Programu ya Uwezo (8 Jun 2010)
- Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi (15 Sep 2011)
- Je Watoto Wetu Wanajifunza? Kuhesabu na Kusoma Katika Afrika Mashariki (28 Jul 2011)
- Kiongozi Asiyewajibika tufanyeje? (29 Oct 2010)
- Shule za Sekondari Tanzania: Wanafunzi wengi, fedha kidogo (28 Oct 2010)

