Wananachi watakiwa kufuatilia pesa za shule za sekondari
2 Feb 2011
|
Katika vyombo vya habari
Twaweza Tanzania inashirikiana na shirika la utetezi wa elimu, HakiElimu na Policy Forum kufuatilia utekelezaji wa ahadi ya serikali kupeleka pesa za uboreshaji wa elimu ya sekondari kila shule ya serikali nchini. Ufuatiliaji huo uliozinduliwa jana umeanza baada ya serikali kuahidi kuwa ifikapo Januari 31, 2011 asilimia 40 yaani shilling 10,000 ya fungu la mwaka mzima kwa kila mwanafunzi itakuwa imefika mashuleni tayari. Jumla ya ruzuku ya uboreshaji elimu kwa kila mwanafunzi kwa mwaka ni shilingi 25,000.
Meneja wa Programu wa Twaweza Tanzania, aliyekuwapo katika uzinduzi, Joseph Ngwegwe, amewataka wazazi, jamii kwa ujumla na waalimu kufuatilia mashuleni kujua iwapo pesa zimefika na kutoa taarifa kwa namba maalumu. “Wazazi wanatakiwa kuuliza mashuleni iwapo pesa zimefika, sababu juhudi zao zitasaidia watoto wao kufanya vema katika mitihani, na kupata ujuzi,” alisema. Kusoma taarifa zaidi kuhusu ufuatiliaji huu soma hapa chini
The Citizen (Kiingereza)
Endelea kusoma: Hakielimu policy forum SEDP II Twaweza
unaweza pia kupenda...
- Watoto 43,000 hatarini kufa kwa utapiamlo (22 Apr 2010)
- Guardian la Uingereza: Twaweza na mabadiliko yanayoletwa na raia Afrika Mashariki (13 Apr 2011)
- Nani anajali afya zetu? (2 Nov 2010)
- Unajali elimu ya mwanao? (2 Nov 2010)
- Wabunge watano wang'ara (20 Oct 2010)
- Wahitimu darasa la saba hawajui kusoma hadithi (25 Sep 2010)
- Wahitimu darasa la 7 hawajui kusoma (25 Sep 2010)

