Uwezo yatambuliwa magazeti ya Tanzania, Guardian la Uingereza, na katika Mkakati Mpya wa Benki ya Dunia kwa Afrika
18 Mar 2011
|
Vyombo vya habari
Uwezo inaendelea kutambuliwa kambi namna inayofaa kuwashiriksha raia kuboresha uwajibikaji katika utoaji huduma kwa umma. Uzinduzi wa utafiti wa Uwezo kwa 2011 jijini Dar es Salaam hivi karibuni umeripotiwa kwenye magazeti la Nipashe, Guardian na Daily News, ambayo yanaeleza ubora wa utafiti wa Uwezo. Blogu ya Povertymatters ya gazeti la Guardian la Uingereza inasema Uwezo imeweka bayana viwang vya chini vya ujifunzaji nchini Kenya, Uganda na Tanzania, na inaihusisha Uwezo na Aser ya India, ambayo ilitoa mawazo na kusaidia kuanzishwa kwa Uwezo Afrika Mashariki. Uwezo pia imetajwa kwenye Mkakati Mpya wa Benki ya Dunia kwa Afrika kama mfano jinsi ambavyo Benki hiyo ingependa kuona sauti za raia na uwajibikaji ukiimarishwa.
Endelea kusoma: Uwezo vyombo vya habari Wabia wa Twaweza
unaweza pia kupenda...
- ShujaazFM yashinda tuzo Maalumu ya One World Media (20 May 2011)
- Guardian la Uingereza: Twaweza na mabadiliko yanayoletwa na raia Afrika Mashariki (13 Apr 2011)
- Envaya ndani ya Forbes (18 Mar 2011)
- Vipindi vya Makutano-Junction na Twaweza vyaanza kurushwa na Citizen TV (18 Mar 2011)
- Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi (15 Sep 2011)
- Ripoti mpya ya Uwezo yapiga mbiu Afrika Mashariki (15 Jul 2011)
- Uwezo Kenya kuzindua ripoti ya upimaji ya mwaka 2011 (20 Jun 2011)

