Je Watoto Wetu Wanajifunza? Kuhesabu na Kusoma Katika Afrika Mashariki
Ripoti muhimu sana imezinduliwa Jumatatu ya Julai 2 jijini Dar es Salaam. Ripoti ya Uwezo ya Afrika Mashariki, kwa mara ya kwanza ina data zinazolinganisha ujuzi wa Hisabati na Ufahamu kwa Kiswahili na Kiingereza kwa nchi tatu za Afrika Mashariki. Sampuli iliyotumika kwenye utafiti huu, kaya 80,000, ni kubwa ya aina yake. Matokeo ya utafiti huu yanatoa picha halisi ya msingi na utayari wa raia wa Kenya, Uganda na Tanzania kustawi na kushiriki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Je kila nchi imefanikiwaje kwa kulinganisha na malengo yake husika? Na, kila nchi inafanyaje ikilinganishwa na nyingine? Na je, matokeo yanatoa picha gani pale uchambuzi wa madaraja tofauti ya kipato cha familia yanapochunguzwa? Ni vigezo vipi huleta mafanikio? Ripoti hii inajibu maswali haya na kutoa ufafanuzi zaidi. Isome hapa.
Endelea kusoma: education Uwezo East Africa Uwezo East Africa Report 2011
unaweza pia kupenda...
- Shule za msingi za Serikali Dar es Salaam:Vyoo vibovu, michezo kidogo. (2 Jun 2011)
- Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam:Msongamano wa wanafunzi bila vitabu vya kiada vya kutosha (2 Jun 2011)
- Matokeo yakipuuzwa, ukaguzi wa nini? (24 May 2011)
- Wabunge waongeaji Bungeni ndio hutetea viti vyao tena? (14 Apr 2011)
- Je, watoto wetu wanajifunza? (22 Sep 2010)
- Programu ya Uwezo (8 Jun 2010)
- Dar es Salaam wanachukuliaje utawala? (19 Dec 2012)

