Twaweza.org

Mwanzo

Twaweza ni nini?

Twaweza ni kusema kwamba tunaweza kufanya mambo yakawa. Hii ni jitihada mpya inayomlenga raia na inayokusudia kuleta mabadiliko makubwa Afrika Mashariki. Twaweza inaamaini kwamba mabadiliko ya kudumu hayana budi kuanzia chini kwenda juu. Tumedhamiria kujenga mazingira na kupanua fursa ambazo zitatoa mwanya kwa mamilioni ya watu kuhabarishwa and kuwawezesha kuweza kuleta maendeleo katika jamii zao moja kwa moja na kuifanya serikali iwajibike. Soma zaidi.

JiElimishe | Uhusiano kati ya matokeo ya kujifunza na utapiamlo

Takwimu mpya zilizotolewa na Uwezo (iliyopo Twaweza) zinaonesha uhusiano kati ya matokeo ya watoto ya kujifunza na utapiamlo. Endelea kusoma...

Fedha, fedha, fedha! Wananchi na huduma rasmi za kifedha.

Maoni ya wananchi kuhusu hali ya fedha nchini. Endelea kusoma...

Wananchi wanasemaje kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania?

Wananchi 7 kati ya 10 wangependa vyombo vya habari vitangaze maovu ya serikali ila 3 kati ya 10 wanahofia utoaji wa taarifa hizo utaathiri nchi. Endelea kusoma...

Hali Halisi: Maoni ya wananchi juu ya elimu bila malipo ya ada.

Maoni ya wananchi kuhusu hali ya elimu nchini Tanzania ndani ya mwaka mmoja uliopita; hasa juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha elimu kwa kuongeza madawati, elimu bila malipo na ruzuku zinazotumwa moja kwa moja mashuleni. Endelea kusoma...

Demokrasia, udikteta na maandamano: Wananchi wanasemaje?

Demokrasia na uhuru wa kutoa maoni ni vitu viwili vinavyothaminiwa sana na wananchi. Asilimia 95 ya wananchi wanauthamini uwezo wa kuikosoa serikali pale wanapoona imekosea. Na asilimia 69 wanakubali kuwa demokrasia ni mfumo bora wa utawala. Endelea kusoma...

Rais wa watu? Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano

Maoni ya wananchi katika miezi ya awali ya uongozi wa Rais Magufuli. Je, ni vitendo gani vya Rais ambavyo vimejipatia umaarufu mkubwa? Na je, wananchi wanaona mabadiliko yoyote kwenye utendaji wa serikali? Endelea kusoma...

Iambie serikali unataka ikufanyie nini!

Tanzania ni moja kati ya nchi 63 zinazotekeleza Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership) Serikali iko katika mkakati wa kutafuta maoni juu ya Mpango Kazi huu wa awamu ya tatu. Endelea kusoma...

Je, watoto wetu wanajifunza?

Baadhi ya watoto wa darasa la 7 hawawezi kufanya majaribio ya darasa la 2. Endelea kusoma...

Nyota njema huonekana asubuhi: Maoni ya wananchi kuhusu huduma za afya

Wananchi wanao ufahamu kuhusu ubora na upatikanaji wa huduma za afya pamoja na wahudumu wake ambao umeongezeka tangu 2015 kutokana na ripoti za wananchi. Endelea kusoma...

Machapisho

Iliyovutia


  • Shindano! Kila robo ya miaka 2013 - kompyuta ndogo (laptops) ishirini zitatolewa kwa washindi na kwa shule watakazozichagua. Toa maoni yako kuhusiana na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii kushinda kabla ya tarehe 1 Novemba 2013. Endelea kusoma...




  • Twaweza imeanzisha kitengo cha Uwazi ambacho kinawapa wabia wa Twaweza, vyombo vya habari na mawakala wakuu wa mabadiliko (wabunge, waandishi wa habari, wakuu wa serikali) taarifa zilizojengwa juu ya msingi wa takwimu, na zinazowasilisha ujumbe ulio ... Endelea kusoma...