Afya

< iliyopita 1 ifuatayo >
4 makala
Sort by: Maoni |

Tanzania: Afya Kwanza

Benki ya taarifa 30 Aug 2017 | Afya

Wananchi wanapopata majeraha ama kuugua, 6 kati ya 10 (61%) huenda katika kituo cha afya cha serikali. Kiwango hiki kimeongezeka kutoka 45% mwaka 2014 na kubaki hivyo hivyo tangu mwaka 2016. Kwa kiasi kikubwa hii imesababishwa na kupungua kwa watu wanaojitibu wenyewe kwa kwenda kwenye maduka ya dawa (9%), maduka ya kawaida kupata dawa (7%), wasiofanya chochote (1%) au wanaotafuta aina nyingine za matibabu (5%). Takwimu zilizokusanywa toka mwaka 2014 zinaonesha kupungua kwa matumizi ya njia hizo. Idadi ya wananchi wanaotumia vituo binafsi, vya kanisa ama vya mashirika yasiyo ya kiserikali haijabadilika katika kipindi hiki (16% mwaka 2017).

Nyota njema huonekana asubuhi?

Benki ya taarifa 9 Aug 2016 | Afya

Utafiti wa Sauti za Wananchi wa Twaweza unaonyesha maoni chanya kutoka kwa wananchi juu ya sekta ya afya nchini Tanzania. Kwa mfano, ni asilimia 18 wananchi wanaoripoti kuona upungufu wa madaktari katika vituo vya afya miezi mitatu iliyopita, ukilinganisha na asilimia 43 walioliona tatizo hili mwaka 2015.

Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu?

Benki ya taarifa 5 May 2014 | Afya

Ni mtu 1 tu kati ya watu 20 (6%) mwenye umri zaidi ya miaka 60 na ni mtoto 1 kati ya 5 (18%) mwenye umri chini ya miaka mitano ambao hupata huduma na matibabu bure katika vituo vya afya. Sera ya Nchi inasema kuwa huduma kwa wagonjwa wa nje kutoka makundi haya mawili ni bure, lakini wananchi wanasema kuwa wanatozwa pesa. Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu? Wananchi na watumishi wa afya wazungumzia huduma za afya.

Dawa zipo au zimekwisha?

Benki ya taarifa 19 Sep 2013 | Afya

Familia mbili kati ya tatu nchini Tanzania zinataarifu kwamba walau mtu mmoja katika familia hizo aliugua katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Ingawa ushauri na tiba ya mwanzo vinaweza kupatikana kwenye maduka ya dawa, wengi wao huishia kutafuta tiba katika kituo cha afya. Je, wagonjwa wanaweza kupata dawa wanazozihitaji katika vituo hivi? Je, ni mara ngapi taarifa kuhusu ukosefu wa dawa hutolewa? Muhtasari huu unatoa taarifa kuhusu maswali haya na mengineyo kuhusu upatikanaji wa dawa nchini Tanzania. Aidha, muhtasari huu, unatoa takwimu za hivi karibuni kabisa kuhusu upatikanaji wa dawa kutoka katika vituo vya afya na kwa wagonjwa waliohojiwa.

< iliyopita 1 ifuatayo >
4 makala
Sort by: Maoni |