Twaweza.org

Ahadi za Sera Bora: Je Serikali ya Uganda ina nia ya dhati

Gazeti la kila wiki la Uganda, The Independent, na la kila siku la New Vision yote yanachapisha maoni ya uchambuzi yalioandikwa na Morrison Rwakakamba, Meneja wa Twaweza Uganda.

Katika uchambuzi huo, Morrison anaonesha mashaka yake kuhusu utashi wa Serikali ya Uganda kutekeleza ahadi zake za sera za kuwa wazi kwa raia wake. Uganda inazo sifa za kuingia kwenye Ushirikiano wa Serikali zilizo Wazi(OGP) lakini haikufanya hivyo  OGP ilipozinduliwa Septemba 2011 huko New York. Zaidi ya hayo, mwandishi anadai kuwa Serikali haijatimiza ahadi ya uwazi na uwajibikaji katika udhibiti wa fedha za umma, ahadi ambazo ni pamoja na uwazi katika kutoa misamaha ya kodi na kutoa machapisho ya hesabu za Serikali.

Makala inaendelea kuhoji jinsi gani Serikali inajiandaa kutimiza ahadi zake za sasa za uwazi na kufanya kila inachodai itafanya kwa raia wa Uganda. Soma zaidi.

 

 

Endelea kusoma: Afrika mashariki

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri