Twaweza.org

Bango la taarifa za bajeti Tanzania lazinduliwa

Uwazi iliyopo Twaweza imezindua bango la mtandaoni kuwezesha taarifa za bajeti kusomeka kwa uwazi na urahisi. Lengo ni kuwezesha matumizi ya pesa za umma—toka kwa walipa kodi na wahisani—kueleweka na kupatikana. Inamaanisha raia, waandishi wa habari, wabunge na ASIZE sasa wanaweza kujua jinsi pesa zinavyotumika, na kuweza kuhoji. Taarifa hizo zitaweza kuonekana kwa namna anuwai.

Inaweza kuoneshwa kama matumizi ya jumla ama wastani kwa kila raia kwa kila mkoa katika sekta tofauti. Akionesha bajeti kwa wastani wa kila mtu, msomaji anaweza kujua kiasi gani cha fedha Hazina imetenga kwa kila raia kwenye elimu, maji na afya. Akibofya kwenye mkoa Fulani kwenye ramani iliyomo kwenye bango matumizi kwa kila wilaya za mkoa huo yataonekana.

Kwenye bango  hili, taarifa za mahesabu zinatokea kama Maputo ya hewa. Mduara mkubwa wa puto kubwa huonesha fedha nyingi. Pia taarifa zaweza onekana kwa mtindo wa tofauti. Taarifa zaweza kuchapwa ama kuhifadhiwa kutoka kwenye bango hili.

Taarifa mpya zitawekwa kwenye bango mara kwa mara ili kwamba habari za bajeti ya Serikali zipatikane kwa raia na wadau wote wanapenda kufuatilia bajeti ya taifa. Kwa sasa bango linazo taarifa za bajeti ya mwaka wa fedha 2009/10 na 2010/2011.

Unaweza kuliona bango la bajeti  hapa. Kwa taarifa zaidi wasiliana na Rose Aiko, Mchambuzi Tafiti, Uwazi, raiko@twaweza.org

Endelea kusoma: budget dashboard

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri