Twaweza.org

Wabunge wetu: Je, Waliwajibika?

Swali muhimu kwa mwananchi yeyote Je, Mbunge wangu aliwakilishaje maslahi yangu Bungeni? Njia moja ya kutathmini utendaji wa Wabunge ni kutazama idadi ya ushiriki wao Bungeni.

Muhtasari unaoitwa Je, waliwajibika? Tathmini ya miaka miwili ya Bunge 2010-2012 uliyoandaliwa na Twaweza kwa kushirikiana na Centre for Economic Prosperity (CEP). Muhtasari unachambua data zinazopatikana kwenye tovuti ya Bunge, kuhusu ushiriki wa kila Mbunge wakati wa vikao vya Bunge. Bunge ndio mhimili wa demokrasia, likiwakilisha wapiga kura katika namna wanavyohusiana na dola. Twaweza na CEP zinatoa tathmini ya utendaji wa Wabunge kwa ujumla, kwa kila chama, kwa kila Mbunge na kwa aina ya ushiriki.

Uchambuzi umeonyesha kwamba Wabunge wanaotoka katika vyama vidogovidogo na vyenye viti vichache huwa na wastani wa juu zaidi wa ushiriki. Tathamini hii inazingatia ushiriki uliofanywa na Wabunge katika miaka miwili ya kipindi cha ubunge cha 2010 – 2015. Wabunge wanaweza kushiriki kwa namna tatu: kwa kuuliza maswali ya msingi, maswali ya nyongeza na kutoa michango. Katika namna zote hizi, TLP ambacho kina mbunge mmoja na NCCR-MAGEUZI watano, , vilikuwa na kiwango kikubwa zaidi chaa ushiriki kwa Mbunge. Hata hivyo, ukiondoa vyama vidogovidogo vyenye chini ya asilimia 5 ya uwakilishi Bungeni, Chadema kinafanya vema zaidi, kikifuatiwa na CUF na CCM.

Wabunge watano walioongoza kwa ushirikiWabunge waliotoa mchango kidogo zaidi Bungeni

Endelea kusoma:

Authors: Thomas Maqway

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri