Twaweza.org

Tunatafuta kazi za sanaa: Mashindano ya Sanaa - Demokrasia na Sanaa


Mnamo Novemba 2017, Twaweza itakuletea “Demokrasia Yetu” - majadiliano ya wazi juu ya demokrasia na nafasi za kiraia nchini Tanzania. Mitazamo tofauti tofauti yatawasilishwa na kuwekwa pamoja kwa lengo la kuhamasisha watu na kujaribu kujenga nafasi za ushirikiano. Tukio hili litatumika pia kusherehekea uwepo wa maeneo ya kidemokrasia na uhuru nchini Tanzania kwa njia ya sanaa.

Twaweza kwa ushirikiano na Nafasi Art Space wanafuraha ya kukutangazia Mashindano ya Sanaa pamoja na Maonyesho yatakayo ambatana na tukio hilo. Tunawasisitizia wasanii wawasilishe kazi zao za sanaa (za aina yoyote - uchoraji, uchongaji, picha, sanaa za video, na installation) zinazojibu au kuchunguza mandhari na mada ya tukio hilo. Haya yataambatana na kujadili uwazi (na usiri), kutenda kwa pamoja (uhusiano mzuri kati ya serikali na wananchi), kubadilishana mawazo kwa uhuru (uwazi kwa mawazo mapya, kukosoa kwa lengo la kujenga, na ushirikiano wakipekee).

Tuzo za washindi zitajumuisha makazi ya wasanii ya muda katika Nafasi Art Space (i.e. artist residencies), na kompyuta (laptop).

Mahitaji ya kuwasilisha
1. Maelezo ya Msanii.
2. CV ikiambatanishwa na taarifa za msanii, elimu, maonesho ya sanaa na tuzo zilizoshindwa (ukurasa 1).
3. Picha 1-3 zenye viwango vizuri za kazi za sanaa zinazo jibu mandhari zikiambatanishwa na maelezo ya sanaa (jina la kazi ya sanaa, mwaka wa uzalishaji, aina ya sanaa na ukubwa wa kazi), kabla ya tarehe 13 Novemba 2017 kumalizika.
4. Msanii lazima alete kazi zake binafsi Nafasi Art Space, Mikocheni B, kati ya 13-17 Novemba 2017.

Muhimu: Mawasilisho katika muundo wa PDF tu yatakubaliwa. PDFs zitumwe mwisho tarehe 13 Novemba 2017 kwa anwani ya barua pepe ifuatayo: asteria@nafasiartspace.org

Soma hapa kwa taarifa zaidi.

Endelea kusoma: demokrasia

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri