Twaweza.org

Mkutano wa Uwazi-Afrika Unalenga Kuleta Demokrasia kwenye Masuala ya Data

Mkutano wa Uwazi-Afrika ulifanyika Zanzibar kuanzia tarehe 7 hadi 8 Oktoba, 2012. Mkutano huo ulijikita kwenye uwazi wa data barani Afrika mada mbalimbali ziliwasilishwa na baadhi ya wanazuoni  muhimu katika uwanja huo wa data, miongoni mwao walikuwa Amadou Mahtar Ba wa Africa Media Initiative, Jay Bhalla wa the Open Institute na Alex Howard wa O’Reilly Media. Mkutano ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba Angela Kairuki aliyetoa mada kuhusu uongozi wa serikali katika ushirikiano na Serikali Uwazi (Open Government Partnership) na vilevile hotuba kuu ya ufunguzi ilitolewa na January Makamba, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Rakesh Rajani wa Twaweza alizungumza katika mkutano huo kuhusu ubunifu unaowagusa watu (Human Centred Design), na aliwapatia washiriki miongozo muhimu ya kuunda na kutekeleza kwa mafanikio miradi ya kiteknolojia yenye kuleta tija kwa watu. Akitolea  mifano ya miradi miwili iliyoshindwa iliyofadhiliwa na Twaweza -- Huduma na Daraja –Rajani alisisitiza mchakato wa usanifu unaoanza na watumiaji pamoja na wengine wanashikishwa kwenye hatua za mchakato  na kisha kufanya kazi kurudi nyuma hadi kufikia mafanikio. Vile vile, alisisitiza dhima ya kuwa tayari kuthubutu  na kushindwa, akieleza kwamba "si suala tu la kufanya kazi kwa bidii ili kupata muundo ulio kamili palepale mwanzoni, bali ni suala la kuunda modeli zilizo nyepesi kurekebishwa, kupimwa ili kuona ufanisi wake na hasa katika kubadilishika kwake kwa haraka ili kupata maoni, kuongeza ubora, na kufanya uendane na mahitaji, lakini pia kujaribu  kitu kipya”.

Mkutano huo uliandaliwa na the Open Institute na Africa Media Initiative, na kupata ufadhili wa Twaweza na makundi mengine. Twaweza inafanya majadiliano na makundi haya kuhusu namna gani demokrasia inaweza kuletwa kwenye data na kuwawezesha wananchi kuzitumia ili kuleta mabadiliko . Vile vile Twaweza imemkaribisha  rafiki mmoja wa kutoka Code4Kenya katika ofisi zake za Nairobi.

Majadiliano katika mkutano huo yalirushwa na washiriki kadhaa kwa njia ya twita na, mmoja wao akiwa Al Kags blog ambaye alichapisha baadhi ya mijadala kwa kina zaidi kidogo kuhusu siku za mwanzo za Mkutano huo. Ripoti ya Mkutano huo itachapishwa hapa (kwa Kiingereza) siku chache zijazo.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri