Twaweza.org

Hivos Yaipongeza ShujaazFM

Mojawapo wa mashirika wafadhili wa Twaweza, Hivos, limepongeza mradi wa ShujaazFM kwa kupokea Tuzo ya OneWorld ya Vyombo Habari Mahsusi kwa jinsi inavyowafikia mamilioni ya vijana nchini Kenya.ShujaazFM ambao ni mbia wa Twaweza hugawa nakala 600,000 za kitabu cha vikaragosi, hutangaza kila siku redioni, hufanya mijadala ya mitandao na kutuma jumbe za simu za mkononi kuwatia moyo na shime vijana wa Kenya wachukue hatua kuboresha maisha yao kwa kujihusisha na masuala halisi yanayohusu mustakabali wao. Makala hiyo pia itakuunganisha na mahojiano na Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Bwn. Alan Duncan, ambaye anaipongeza kazi ya ShujaazFM kwenye tafrija ya kutoa zawadi za OneWorld Media jijini London mapema mwaka huu. Soma zaidi.

Endelea kusoma: agency

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri