Twaweza.org

Jinsi mabadiliko yanavyotokea

Jinsi mabadiliko yanavyotokea

Twaweza imeanzishwa kutokana na kuatambua kwamba tunahitaji zaidi ya maamuzi yanayotoka juu kwenda chini—tunahitaji ushiriki na usimamizi wa wananchi. Twaweza inaamini kwamba wananchi weledi na waliohamasika   ni chembechembe zenye nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko endelevu, Tunauona utashi wa kutenda wa wananchi kama lengo linalojitegemea, lakini pia kama njia inayoweza kusababisha uboreshaji wa huduma na usimamizi bora wa rasilimali za umma. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, wananchi walio wengi hukosa taarifa na fursa wanazohitaji ili waweze kuiwajibisha serikali yao.

Kwa hiyo, Twaweza inalenga kuwawezesha mamilioni ya raia wa Afrika Mashariki kufanya yafuatayo :

  • kuhabarishwa – kwa kupanua nyenzo na mitandao ambayo wananchi wanaweza kuipitia kupata habari, Twaweza inalenga kuwawezesha wananchi :
  • kutumia utashi wao wa kutenda –  kutoa maoni yao, kuchukua hatua za kuboresha maisha yao na kuiwajibisha serikali : kwa hiyo, Twaweza inakusudia kuwawezesha wananchi :
  • kupata huduma za msingi zilizo bora (elimu ya msingi na sekondari, huduma ya afya ya msingi na maji safi) na waweze kuwa na udhibiti mkubwa zaidi juu ya rasilimali zinazohusika katiak utoaji wa huduma.

Endelea kusoma: mabadiliko

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri