Twaweza.org

Ufafanuzi kuhusu Matokeo ya Kidato cha Nne

Kwa wiki kadhaa, Twaweza na Mkuu wa shirika letu, Rakesh Rajani, tumepokea maombi mengi ya kutaka ufafanuzi kuhusiana na Matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne 2012, na juu ya uamuzi wa Serikali kupanga upya matokeo hayo. Kwa sehemu, hamasa hii imetokana na Waziri Mkuu kumteua Nd. Rajani kuwa mjumbe wa Tume ya kuchunguza sababu za matokeo mabaya. Kwa taarifa, ifahamike kwamba Nd. Rajani aliomba kutoendelea kushiriki kwenye Tume baada ya kumaliza muda wake wa awali wa majuma sita. Kwa manufaa ya uwazi, leo tunaiweka wazi barua aliyomtumia Waziri Mkuu kuhusiana na mapendekezo ya awali ya Tume na maamuzi yaliyochukuliwa na Serikali. Tunaamini hili litachangia katika mjadala wa umma unaoendelea kuhusu uboreshaji wa elimu nchini.

Kusoma barua bofya 'Barua kwa Waziri Mkuu' chini ya 'Pakua Nyaraka'

Endelea kusoma: elimu

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri