Twaweza.org

Kuhusu Twaweza

Twaweza ni asasi huru ya Afrika Mashariki iliyoanzishwa mwaka 2009 na Rakesh Rajani, Mtanzania ambaye ni kiongozi wa asasi za kiraia na pia ndiye aliyeanzisha HakiElimu na akaiongoza kama mkurugenzi mtendaji wa kwanza hadi mwishoni mwa mwaka 2007. Mtazamo wa Twaweza na fikra yake kuhusu mabadiliko vimejengeka juu ya misingi ya mafunzo yaliyopatikana kutokana na uzoefu wa HakiElimu, pamoja na majadiliano mapana ndani ya Afrika Mashariki yaliyofanyika mwaka 2008, na vile vile baada ya mapitio ya maandiko mengi. Hivos ilisaidia kwa kuipa Twaweza mahali pa awali pa kuanzia shughuli zake, na hadi hivi sasa bado inaendelea kuihifadhi hadi hapo Twaweza itakapoweza kwenda peke yake ifikapo mwaka 2013. Hivos imesajiliwa katika nchi za Afrika Mashariki kama kampuni isiyofanya faida (isiyo na mitaji ya hisa).  

Mtazamo wa Twaweza, pamoja na sera zake, mifumo yake na taratibu zake ni vielelezo vya maadili ya msingi yahusuyo utawala wa uwazi ulio makini. Maeneo matano ya maadili hayo ndiyo yanayoongoza kazi zetu: Umakini na uwajibikaji; uwazi na mawasiliano; maadili ya uongofu; tafakuri na kujifunza; na uwajibikaji na ubebaji wa majukumu. Soma zaidi kuhusu maadili yetu

Wafadhili wetu

Twaweza inaungwa mkono na mkusanyiko wa wafadhili watano ambao wanatoa misaada ya muda mrefu kwa ajili ya ujumla wa programu yetu. Hawa ni Sida, DFID, Hewlett Foundation, SNV na Hivos. Twaweza huwasilisha taarifa ya pamoja ya mwaka na ya nusu-mwaka kwa wafadhili wote.

Bajeti ya Twaweza

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri