Mada Moto Moto

< iliyopita 1 ifuatayo >
7 makala
Sort by: Maoni |

Uchungu wa Njaa

Benki ya taarifa 1 Mar 2017 | Mada Moto Moto

Idadi kubwa ya wahojiwa wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) wameripoti uhaba wa chakula katika maeneo wanayoishi. Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini ambako asilimia 84 wameripoti uhaba wa chakula ikilinganishwa na asilimia 64 katika maeneo ya mijini.

Fedha, fedha, fedha!

Benki ya taarifa 15 Dec 2016 | Mada Moto Moto

Maoni ya wananchi kuhusu hali ya fedha nchini.

Matarajio lukuki

Benki ya taarifa 2 Sep 2015 | Mada Moto Moto

Wananchi wengi hawana taarifa sahihi kuhusu gesi asilia iliyogundulika hivi karibuni nchini Tanzania. Asilimia 53 wanafikiri kuwa gesi iliyogunduliwa pwani ya Tanzania tayari inavunwa na inazalisha mapato (makadirio yanaonesha kuwa hadi mwaka 2025 ndipo gesi itakapoanza kuvunwa). Pia, wananchi 6 kati ya 10 wanaamini kuwa Serikali na makampuni ya kigeni tayari yameshaanza kuingiza mapato kutokana na gesi hii (kitu hiki kitawezekana pale ambapo gesi itaanza kuvunwa kwa ajili ya matumizi).

Tanzania ifikapo mwaka 2025

Benki ya taarifa 4 Dec 2014 | Mada Moto Moto

Zaidi ya nusu ya wananchi (54%) wanafikiri kuwa maisha yao yatakuwa bora zaidi ifikapo mwaka 2025. Huu ndio mtazamo wa wananchi wakio katika makundi yote- vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake, na wakazi wa vijijini na mijini.

Hima tujenge nyumba moja

Benki ya taarifa 6 Oct 2014 | Mada Moto Moto

Wananchi wanane kati ya kumi (80%) wanafikiri kuwa Tanzania inapaswa kubakia ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Aidha, wananchi tisa kati ya kumi (85%) wanakubali uwepo wa ushirikiano mkubwa zaidi na Kenya na Uganda.

Kusimamia Maliasili

Benki ya taarifa 2 Jun 2014 | Mada Moto Moto

Wananchi wanne kati ya watano wanaamini kuwa mafuta na gesi yatawanufaisha wao, watoto wao na nchi yao kwa ujumla. Wakati huo huo, wananchi wanne kati ya kumi (37%) wanaamini kuwa viongozi wa Serikali na matajiri ndio wataofaidika zaidi. Pia, zaidi ya nusu (55%) wangependa baadhi ya mapato ya mafuta na gesi wapewe wananchi moja kwa moja kama fedha taslimu.

Je, Tuko Salama?

Benki ya taarifa 4 Mar 2014 | Mada Moto Moto

Karibu nusu (46%) ya Watanzania wote wamearifu kuwa wameshawahi kushuhudia vurugu katika jamii katika kipindi cha miezi sita iliyopita, ikilinganishwa na idadi ya mtu 1 kati ya 5 (20%) anayeripoti kuwa amewahi kuibiwa kitu na wezi. Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti.

< iliyopita 1 ifuatayo >
7 makala
Sort by: Maoni |