Twaweza.org

Viongozi wakutana kuadhimisha mwaka mmoja wa Ushirikiano na Serikali Wazi

Maadhimisho ya mwaka mmoja ya Serikali kwa Uwazi (unaofahamika kama OGP)  yalifanyika jijini New York wakati Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ukiendelea. Maadhimisho hayo ya kwanza yalihudhuriwa na watu wengi maarufu na kupokewa kwa shauku kubwa ambapo hotuba za viongozi mbalimbali wa OGP na wawakilishi wa taasisi muhimu za kiraia zilitolewa. Tukio hilo pia lilishuhudia kuzinduliwa kwa Mfumo Huru wa Utoaji Taarifa (IRM) – unaoundwa na jopo la a watu maarufu na wataalamu wa sera katika ngazi ya kimataifa walio na uzoefu mkubwa  – ambao watafuatilia maendeleo na kuhakikisha kuna uwajibikaji mkubwa  wa Serikali zinazoshiriki kwenye mpango wa OGP. Wakati wa tukio hilo, Uingereza na Indonesia zilichaguliwa kushika kiti cha Uenyekiti wa OGP, pamoja na mwenyekiti mwenza wa asasi za  kiraia Warren Krafchik kutoka International Budget Partnership (Ushirika wa Kimataifa katika masuala ya Bajeti).

Katika maadhimisho ya mwaka mmoja, Tanzania iliwakilishwa na Waziri Chikawe, ambaye ndiye kiongozi wa OGP nchini, na Mkuu wa Twaweza, Rakesh Rajani, ambaye alitoa hotuba ya kufunga. Akieleza kwamba OGP ingeweza kutoa mwanya kama Serikali zitajipanga kuwajibika kwa raia, Rajani alisisitiza “[Tunahitaji] kuibua njia mpya ya ushirikiano katika kuendesha Serikali, njia ambayo haihimizi tu kutoa amri (na maelelezo) bali inayoweka mazingira ya Serikali na raia kuungana na kutatua matatizo ya jamii nzima.”

Katika mwaka wake wa kwanza, OGP imeonesha kwamba duniani kote kuna nia ya kuzifanya Serikali ziwe wazi zaidi. Lakini, kwa mujibu wa washiriki wengi waliohudhuria maadhimisho hayo ya kwanza, wakati wa kutoa maazimio ulikuwa umekwisha, na sasa ilikuwa ni wakati wa vitendo na uwajibikaji. Wananchi ulimwenguni kotewanatazama yanayoendelea,  ni suala la muda tu ambapo itadhihirika kama kweli OGP imeweze kufikia matarajio.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri