Mwanzo
Twaweza ni nini?
Twaweza ni kusema kwamba tunaweza kufanya mambo yakawa. Hii ni jitihada mpya inayomlenga raia na inayokusudia kuleta mabadiliko makubwa Afrika Mashariki. Twaweza inaamaini kwamba mabadiliko ya kudumu hayana budi kuanzia chini kwenda juu. Tumedhamiria kujenga mazingira na kupanua fursa ambazo zitatoa mwanya kwa mamilioni ya watu kuhabarishwa and kuwawezesha kuweza kuleta maendeleo katika jamii zao moja kwa moja na kuifanya serikali iwajibike. Soma zaidi.
Taarifa kuhusu Muswada wa Marekibisho ya Sheria Mbalimbali (Miscellaneous Amendments) No. 3 (2020)
Marekebisho mengi yanayopendekezwa yanakiuka maana na dhamira ya Katiba yetu. Mapendekezo haya yanahatarisha misingi muhimu kabisa ya Katiba kama vile usawa mbele ya sheria (Ibara ya 13), Katiba kuwa ndio sheria kuu (Ibara ya 26), na mgawanyo wa mada...
Endelea kusoma...
Ndoa za Utotoni Hupunguza Ubora wa Maisha kwa Wasichana wadogo na Watoto wao
Nchini Tanzania, wasichana 2 kati ya 5 wameolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18. Nchi inaweza kuwa inapoteza kiasi cha Tsh milioni 637 kila mwaka (ilikadiriwa, 2015) mapato yanayopotea kwasababu ya ndoa za utotoni.
Endelea kusoma...
Wanawake wa Mwanga Kusini, Kigoma wanakabiliwa na ubakwaji na ukatili
Wanawake wengi wa Kigoma wanaishi kwa hofu tangu mwaka 2016 kutokana na uhalifu unaojulikana kama Teleza. Wanawake, hususan wale wanaoishi bila wanaume katika nyumba zao, wako kwenye hatari ya kuvunjwa kwa nyumba zao na watu wasiojulikana kisha kubak...
Endelea kusoma...
Tamko kuhusu Marekebisho yanayopendekezwa kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa
Sisi kama taasisi huru ya kiraia ambayo inalinda haki/kanuni za kidemokrasia, tungependa kutoa maoni na kupaza sauti yetu kwenye mjadala unaoendelea tukiwa na lengo la kutafuta njia bora ya kusonga mbele, ambayo italinda demokrasia yetu changa huku i...
Endelea kusoma...
Tukiwathamini walimu, lengo la elimu bora litatimia
Inashangaza kuona jamii ya sasa inamchukulia mwalimu kama mtu aliyeshindwa kufanya/kupata kazi nyingine ndio akakimbilia ualimu. Mwalimu ni mtu anayetafsiriwa kuwa anaishi maisha ya duni, ya kubangaiza huku akisongwa na madeni lukuki.
Endelea kusoma...
Maoni kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu
Kama mdau muhimu katika tafiti huru na ukusanyaji wa takwimu, Twaweza iliwasilisha uchambuzi wa marekebisho yanayopendekezwa ya Sheria ya Takwimu (2015). Mtazamo wetu.
Endelea kusoma...
Maelezo mafupi kutoka Twaweza
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza sio mwanachama na hajawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini Tanzania.
Endelea kusoma...
Twaweza ni nani?
Kwa wiki kadhaa zilizopita, Twaweza imetajwa sana na kujadiliwa katika vyombo vya habari na katika mijadala mbali mbali ya umma.
Endelea kusoma...
Maelezo mafupi kuhusu barua kutoka Costech kwa Twaweza
Twaweza haijasambaza, na haihusiki na usambazaji wa barua hiyo kwenye mitandao ya kijamii. Tunayaheshimu sana mawasiliano yetu na washirika wetu.
Endelea kusoma...