Twaweza.org

Kuongeza fedha pekee hakusaidii kumaliza tatizo la uhaba wa dawa

Licha ya ukosefu wa fedha za kutosha katika sekta ya afya, tatizo la kuisha kwa akiba ya dawa katika vituo vya afya halitotatuliwa kwa kuongeza rasilimali peke yake. Utafiti mpya uliofanywa na Twaweza kwa kushirikiana na Shirika la Overseas Development Institute (ODI) limechambua sababu za uhaba wa dawa na kupendekeza mbinu za kutatua tatizo.

Tanzania inakabiliwa na vikwazo vikubwa kwenye bajeti za afya. Kwa mfano, bajeti kwa ajili ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka 2012-13 ilikuwa ni shilingi bilioni 80 kinyume na makadirio ya mahitaji ya shilingi bilioni 198. Hata hivyo, uhaba wa dawa hutokea mara kwa mara na husababishwa ya mambo kadhaa, siyo kukosekana kwa rasilimali tu. Mambo yafuatayo yanachangia pia kuendelea kwa tatizo la kuisha kwa akiba ya dawa:

  • Wanasiasa na wananchi wote wanaonekana kupendelea mageuzi ya miundombinu yanayoonekana kwa urahisi kama ujenzi wa zahanati, kuliko maboresho ya kina ya mfumo wa utoaji huduma za afya.
  • Hakuna takwimu za uhakika kuhusu dawa zinavyoagizwa, zinazopokelewa au kutumika. Takwimu zinapopatikana, zinatumika kuripoti kwa wasimamizi badala ya kutumiwa kama zana za kuwasaidia wafanyakazi kusimamia na kuhudumia vyema vituo vya afya.
  • Mambo yanapoharibika, kwa mfano madawa yakipotea, ni hatua ndogo tu au hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kuchunguza au kushughulikia suala hilo. Isitoshe majukumu na wajibu havieleweki vyema miongoni mwa wafanyakazi kujua nani ana wajibu upi. Hata hivyo, baadhi ya Waganga Wakuu wa Wilaya na Mkoa hufuatilia masuala haya na wamepata baadhi ya mafanikio.
  • Ingawa wananchi wanafahamu kuwa kuisha kwa akiba ya dawa ni tatizo, bado hawajui nini cha kufanya kutatua tatizo hili.

Mapendekezo:
Utafiti wa Twaweza na ODI umependekeza njia za kushughulikia tatizo la kukosekana kwa madawa kwenye vituo vya afya vya umma.

  • Wananchi wanaweza kufanya ukaguzi huru wa nini kipo au hakipo katika vituo vya afya vilivopo kwenye maeneo yao. Tafiti kama zile za Uwezo zinazofanyika kwenye elimu, zinaweza pia kufanyika kwenye sekta ya afya.
  • Takwimu kutoka vituo vya afya zinapaswa zitolewe ili wanataaluma, vyombo vya habari na asasi za kiraia ziweze kuchambua na kuwahabarisha wananchi.
  • Viongozi wa afya ambao wanatatua matatizo ni lazima wabainishwe na watambuliwe. 'Siri' ya mafanikio yao inapaswa kutangazwa ili kuchochea wadau wa sehemu nyingine kuiga siri hizo na kuleta mafanikio
  • Viongozi, ikiwa hasa wa wilaya, wanaweza kujifunza kutokana na vituo vya vifaa vilivyofanikiwa kuepusha au kupunguza tatizo la kuisha kwa akiba ya dawa licha ya kukabiliwa na changamoto zinazofanana na maeneo mengine ya nchi. Hawa wanaweza kutoa mawazo ya jinsi za kushughulikia suala hili. Kuwatambua au kuwazawadia kutawapa motisha zaidi ya kuendelea kufanya kazi zao vizuri na kunaweza kuhamasisha wengine kufuata nyayo zao.
  • Serikali inapaswa kushirikiana na wadau wengine ili kwa pamoja waje na ufumbuzi wa kibunifu.

Endelea kusoma: afya

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri