Twaweza.org

Iambie serikali unataka ikufanyie nini!

Tanzania ni moja kati ya nchi 63 zinazotekeleza Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi  (Open Government Partnership). Serikali iko katika mkakati wa kutafuta maoni juu ya Mpango Kazi huu wa awamu ya tatu.  

Moja ya vigezo na matakwa ya utekelezaji ya mpango huu kwa nchi mwanachama, ni kuandaa Mpango Kazi wa Taifa (National Action Plan) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na wananchi. 

Rasimu ya Mpango Kazi kwa mwaka 2016/2017-2017/2018 imeandaliwa. Mpango kazi huo, utahusisha vipaumbele katika maeneo saba ambayo ni Upataji taarifa (Access to information),  Takwimu huria (Open data), Bajeti za wazi (Open budget), Uwazi kuhusu ardhi (Land transparency), Uwazi kuhusu tasnia ya uzinduaji (Extractive Industries Transparency), Uwazi katika masuala ya afya (Medical and Health Service Systems Transparency) na Mifumo ya utendaji kazi (Performance Management).

Hivyo, serikali inawakaribisha wananchi na wadau kutoa maoni na ushauri ili kuboresha Rasimu ya Mpango Kazi wa Kitaifa, hususan katika maeneo yenye upungufu. Njia zinazoweza kutumiwa na wadau ili kuwasilisha maoni yao ni Tovuti Rasmi ya wananchi (www.wananchi.go.tz), tovuti ya OGP (www.opengov.go.tz), Government Open Data Portal (www.opendata.go.tz), kupitia barua pepe (ps@utumishi.go.tz), Katibu Mkuu, Ofisi ya raisi, Menejimenti ya utumishi ya Umma na Kwa njia ya barua kupitia SLP 2483, Dar-Es-Salaam.

Serikali inawahimiza wadau na wananchi kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao. Mwisho wa kupokea maoni, ushauri, mapendekezo kutoka kwa wadau na wananchi ni tarehe 16/09/2016 saa 9:30 Alasiri.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri