Twaweza.org

Serikali inakusanya maoni ya wananchi kuhusu huduma za afya, elimu na maji

Kama sehemu ya mchango wake katika Mpango wa Kimataifa wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP), Twaweza imezindua shindano litakalohusisha utoaji wa kompyuta ndogo (laptops) kwa washindi na kwa shule watakazozichagua. Washindi watakuwa wale watakaotoa maoni bora zaidi kuhusu namna huduma za afya, elimu na maji zinavyoweza kuboreshwa na mwananchi anapaswa kufanya nini kuleta mabadiliko.

Serikali ya Tanzania inakusanya maoni ya wananchi kuhusu namna ya kuongeza ubora, uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma hizo. Twaweza inasaidiana na Serikali katika jukumu hili, kwa kutumia njia ya utayarishaji machapisho-pendwa na kusaidia kupitia maoni hayo.

Kati ya machapisho-pendwa yatakayotumika kuhamashisha shindano hili, ni vijitabu vya vibonzo vilivyoandaliwa kwa kushirikiana na Tamasha. Maelezo yake yanapatikana katika sehemu ya Sherehekea mawazo yako

Rakesh Rajani, Kiongozi wa Twaweza, alisema: “Mpango wa Kimataifa wa Kuendesha Shuguli za Serikali kwa wazi  ni mkabala mpya wa utawala unaozingatia ubia kati ya wale wanaotawala na wale wanaotawaliwa ili kutafuta ufumbuzi kwa changamoto kubwa zaidi zinazotukabili. Kukusanya maoni ya raia kuhusu namna ya kuongeza ubora katika utoaji huduma ni hatua muhimu ya kwanza katika kuhakikisha kwamba dira hii inakuwa kweli na Twaweza inafurahi kuweza kusaidiana Serikali kwa kufanya wito huu kwa watu usambae zaidi ili kukusanya maoni.”  

Shindano hili limezinduliwa kwa tukio maalum lililohudhuriwa na Kiongozi wa OGP Tanzania Mheshimiwa Mathias Chikawe (Waziri wa Katiba na Sheria), Richard Mabala (Mkurugenzi, Tamasha) na John Ulanga (Mkurugenzi Mtendaji, Foundation for Civil Society).

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri