Twaweza.org

Toa maoni, jishindie kompyuta

Ndugu msomaji, hivi karibuni Serikali ya Tanzania imeahidi kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kupitia mpango huu, Serikali inataka kukusikia.

Toa maoni yako kuhusiana na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii; maji, elimu na afya.

Tuambie wazo moja kuboresha elimu, afya au maji. Halafu, tuambie mwananchi afanye nini kuleta mabadiliko.

Kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka 2013, maoni kumi bora yatachaguliwa na kompyuta ndogo (laptops) zitatolewa kwa washindi na kwa shule watakazozichagua. Pia, maoni ya washindi yatachapishwa kwenye vitabu na tovuti.

Tuma maoni yako kabla ya tarehe 1 Novemba, 2013

Anuani: OGP Tanzania, S.L.P 38342, Dar es Salaam
Barua pepe: unasemaje@gmail.com

Kumbuka kuweka taarifa hizi:
Tarehe
Majina kamili, umri wako, jina la shule; jinsia (me/ke)
Anuani kamili: SLP na makazi (kata, wilaya na mkoa); namba ya simu; barua pepe

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri