Twaweza.org

Ripoti mpya ya Uwezo yapiga mbiu Afrika Mashariki

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu amewapa changamoto wadau wa elimu kuboresha kiwango cha elimu ya msingi kwa nchi za Afrika Mashariki iwapo Jumuiya hiyo inataka kushindana kimataifa. Balozi Mwapachu amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye hotuba ya kuzindua ripoti ya elimu kwa nchi za Afrika Mashariki. Ripoti hiyo mpya inaonesha kuwa wanafunzi wa madarasa ya juu ya elimu ya msingi nchini Kenya, Uganda na Tanzania walishinda kufauli majaribio ya darasa la pili.

“Jumuiya hii itayumba katika mipango na matarajio ya malengo yake iwapo kiwango chake cha elimu ya msingi kitabakia hivi kilivyo leo,” amesema Balozi Mwapachu. Unaweza kusoma hotuba yake nzima ukibofya hapa. Fungua ripoti kwenye sehemu ya machapisho.

Endelea kusoma: elimu Afrika Mashariki

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri