Twaweza.org

Ripoti mpya ya Uwezo yapiga mbiu Afrika Mashariki

Vyombo vya habari Afrika Mashariki vimepiga mbiu kutokana na ripoti mpya ya Uwezo Afrika Mashariki kuhusu uelewa wa kusoma na kuandika na Hisabati, Kenya, Uganda na Tanzania mara baada ya ripoti hiyo kuzinduliwa na Katibu Mkuu wa Zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu jijini Dar es Salaam Julai 4. Magazeti mengi yameripoti na kuchambua matokeo ya Uwezo, ambayo yanaonesha umahiri wa hali ya chini wa watoto katika ufahamu na Hisabati. East African linashauri kuwa iwapo mtu anapenda kujiandikisha shule hapa Afrika Mashariki basi akajiandikishe Kenya ambako uelewa wa Kusoma na Kuhesabu ulionekana kuwazidi majirani zake wa Uganda na Kenya. Magazeti mengine yamechukua msimamo tofauti kuhusu ripoti hiyo. The Citizen la Tanzania linaitaka Serikali kutochukia kukosolewa. Tanzania Daima, Nipashe, Mtanzania, The African, Habari Leo na Mwananchi pia zimeripoti kuhusu matokeo mbalimbali ya utafiti huo. The Nation la Kenya linaripoti kuhusu ripoti hiyo. Owen Barder anaaandika kwenye blogu yake kuwa kuna matumaini kwa kuwa baadhi ya wilaya zimefanya vizuri kuliko wilaya nyingine. “Kwa vile sehemu zingine zimefanya vizuri kuliko zingine, inamaanisha kuwa inawezekana kuboresha mambo katika muktadha huo huo ulimofanyika utafiti.”

Endelea kusoma: Elimu ya Msingi meta sticky Uwezo vyombo vya habari Afrika Mashariki vyombo vya habari Kenya vyombo vya habari Tanzania

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri