Twaweza.org

Ripoti ya Uwezo 2011 yatoa mwangwi kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki

Uwezo, jitihada ya miaka minne kuinua viwango vya ufahamu kusoma na kuandika na hisabati kwa watoto wa umri wa miaka 6-16 Afrika Mashariki umezindua ripoti zake za Upimaji wa Kujifunza 2011 nchini Kenya, Uganda na Tanzania mwezi Julai na Agosti. Matokeo kwenye ripoti hizo yanaonesha viwango vidogo vya ujuzi wa hesabu na ufahamu wa kusoma na kuandika miongoni mwa  watoto wa nchi zote tatu.

Magazeti ya Kenya, Uganda na Tanzania yameyapa nafasi matokeo hayo kwenye kurasa zao za habari. Habari na makala zimejadili elimu katika mitazamo tofauti katika nchi hizi huku zikinukuu matokeo yaliyomo kwenye ripoti hizo.

The Guardian la Tanzania linanukuu Ripoti ya Uwezo Tanzania 2011 katika makala hizi:  Miaka 50 ya Uhuru: Elimu ya Kujitegemea bado inafaa? Kushuka kiwango cha lugha ya Kiingereza kikwazo kwa wanafunzi, walimu, Pale taifa linapowanyima watoto wake elimu ya msingi...na Uwezo yatoa ripoti mpya ya inayotisha kuhusu hali ya uelewa mashuleni.

The East African linanukuu matokeo ya ripoti za 2011 za ujifunzaji  za Kenya, Uganda na Tanzania; kisha linahitimisha kuwa watoto wa Afrika Mashariki bado wanaelewa kidogo sana mashuleni.

The Daily News linatumia ripoti ya Uwezo Tanzania kuuliza swali: Je watoto wetu wanajifunza? Kisha, limetoa maoni ya kihariri yanayopendekeza namna ya kutatua tatizo hilo.

The Citizen limenukuu matokeo yaliyomo kwenye ripoti kuonesha jinsi hali ya elimu Tanzania ilivyo mbaya.  

Magazeti ya Kiswahili yakiwamo Habari Leo, Majira na Tanzania Daima yaliandika kuhusu elimu na kunukuu ripoti ya Uwezo 2011.

Unaweza pia kuangalia video hii kuona namna Uwezo Kenya walivyokuwa wakifanya upimaji wa kujifunza.

Endelea kusoma: elimu

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri