Twaweza.org

Ruzuku ya wanafunzi kwa ajili ya Elimu: Ni lini italeta mabadiliko?

Uwazi imetoa uchambuzi mpya wa ruzuku kwa ajili ya elimu ya msingi. Muhtasari huu unaokwenda kwa jina  la "Ruzuku ya wanafunzi kwa  ajili ya elimu: Ni lini italeta mabadiliko?" unaonyesha kwamba kiasi kilichotengwa ni kidogo mno na kimepungua thamani kwa asilimia zaidi ya 35 tangu sera hii ilipoanzishwa mwaka 2002.

Kulingana na sera, ruzuku ilitakiwa kuwa shilingi 10,000 kwa kila mwanafunzi lakini kiasi kamili kamwe hakijawahi kufika mashuleni tangu mfumo huu  ulipoletwa. Uchambuzi unaonyesha kwamba  mfumo huu unahitaji kusukwa upya kabla ya kuleta mabadiliko katika elimu. Habari zaidi juu ya matokeo haya ya utafiti inaweza kupakuliwa hapa chini.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri