Walezi wa uwajibikaji: Ufahamu na maoni ya wananchi kuhusu taasisi za usimamizi
24 Feb 2015
hot
| Machapisho
Wananchi saba kati ya kumi (69%) wanasema rushwa zilizoripotiwa kwenye ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni upotevu wa fedha zao (za umma). Zaidi ya nusu ya wananchi (55%) wanaamini kuwa aina hii ya rushwa inagusa sana maisha ya yao ya kila siku, na watatu kati ya kumi (31%) wangependa kutaarifiwa kuhusu matokeo ya ukaguzi kupitia vipindi vya redio vinavyorushwa kila wiki kwa muda wa nusu saa.
Wananchi pia wanaamini kuwa Rais anapaswa kuchukua hatua juu ya matokeo ya ripoti ya CAG: Takriban wananchi sita kati ya kumi (57%) wanaamini kuwa Rais anawajibu wa kufuatilia masuala ya ukaguzi wa hesabu za serikali. Taasisi nyingine zinazotajwa kuwa na wajibu wa kufanya hivyo ni pamoja na Baraza la Mawaziri (16%) na mahakama (11%). Mbali na Rais, hakuna taasisi au mtu binafsi aliyetajwa na wananchi kwa zaidi ya 20% kuwa anawajibu wa kushughulikia masuala ya ukaguzi wa hesabu za serikali.
Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari mfupi wenye jina la Walezi wa Uwajibikaji: Ufahamu na maoni ya wananchi kuhusu taasisi za usimamizi. Muhtasari huu umetokana na takwimu kutoka utafiti wa Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kwa njia ya simu za mkononi. Matokeo yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,474 katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara (Zanzibar haimo kwenye matokeo haya) kati ya miezi ya Septemba na Oktoba 2014.
Licha ya kuwepo kwa taarifa za wazi juu ya makosa ya rushwa na haja ya Rais kuchukua hatua, wananchi wana hisia kinzani linapokuja suala la adhabu kwa viongozi wenye matumizi mabaya ya fedha za umma. Mwananchi mmoja tu kati ya ishirini (6%) anafikiri kuwa wale wanaopatikana na hatia ya rushwa wanapaswa kuondolewa katika ofisi za umma, na ni mmoja tu kati ya wananchi sita (15%) anayefikiri kuwa wala rushwa wanapaswa kufungwa. Adhabu sahihi kwa wala rushwa iliyotajwa na wananchi wengi (32%) ni kufukuzwa kazi, kunyang’anywa pensheni, kunyang’anywa mafao na kulipa pesa walizofuja (30%).
Endelea kusoma:
Authors: Angela Ambroz
pakua nyaraka
- Walezi wa uwajibikaji | Muhtasari |
1.71 MB
- Wananchi wanaiona rushwa kama upotevu wa fedha zao na wangependa Rais achukue hatua | Taarifa kwa Vyombo vya Habari |
297.19 KB
- Guardians of Accountablity | Muhtasari |
1.72 MB
- Citizens see corruption as loss of their money and want the President to act | Taarifa kwa Vyombo vya Habari |
289.1 KB
Tafsiri
unaweza pia kupenda...
- Matarajio lukuki: Maoni ya wananchi kuhusu sekta ya gesi (31 Aug 2015)
- Ufunguo wa maisha | Maoni ya wananchi juu ya umuhimu wa shule Muhtasari huu (16 Jul 2015)
- Machoni mwa umma: Maoni ya wananchi juu ya upatikanaji wa taarifa (15 Jun 2015)
- Usalama Wetu? Maoni ya wananchi juu ya usalama na haki (28 Apr 2015)
- Kuelekea Kura ya Maoni: Maoni ya Watanzania kuhusu Katiba Inayopendekezwa (1 Apr 2015)
- Tanzania ifikapo mwaka 2025: Je, Watanzania wana matarajio gani na maisha yao ya baadaye? (4 Dec 2014)
- Kulinda haki za kila mtu: Maoni ya wananchi juu ya ulemavu (4 Nov 2014)