Twaweza.org

Wananchi Wazungumza kuhusu Matokeo ya Kidato cha Nne

Wazazi wana ufahamu kuhusu mwendelezo wa kuanguka kwa ubora wa elimu ya sekondari, na kwa kiasi kikubwa wanatupa lawama kwa serikali na walimu kwa kuanguka huko. Wazazi wanaitaka serikali kuongeza idadi ya walimu waliofuzu na wenye sifa stahiki na wanaolipwa vizuri iliwasaidie kuboresha elimu nchini Tanzania.

Matokeo haya yamechapishwa katika muhtasari wa Twaweza unaoitwa Matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Nne: Wananchi wazungumzia mgogoro wa kujifunza Tanzania. Muhtasari huo umeandaliwa kutokana na takwimu zilizokusanywa kupitia utafiti wa Sauti za Wananchi, ambao ni utafiti wa njia ya simu za mkononi wenye sura ya uwakilishi wa kaya kitaifa kote Tanzania Bara. Wahojiwa waliombwa kueleza maoni yao kuhusu elimu, na kubaini changamoto na njia za kuongeza ubora. Takwimu zilizotumika kwenye Muhtasari huu zilikusanywa kati ya tarehe 18 Machi hadi 3 Aprili, 2013 kabla ya tangazo la serikali la kurekebisha matokeo ya Kidato Cha Nne ya mwaka 2012.

Miongoni mwa waliohojiwa, asilimia 68 ya wananchi walikuwa na taarifa kwamba matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne ya 2012 yalikuwa yamechapishwa. Idadi kubwa ya wahojiwa walionesha kutambua kuanguka kwa ubora wa elimu ya sekondari katika miaka kumi iliyopita, ambapo wananchi asilimia 83 walionesha kwamba elimu ilikuwa imeporomoka. Idadi hiyo inaendana na takwimu rasmi zikiwamo zile za Wizara ya Elimu zinazojulikana kama Basic Education Statistics in Tanzania (BEST).

Endelea kusoma: elimu

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri