Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu?
5 May 2014
hot
| Uwazi
Ni mtu 1 tu kati ya watu 20 (6%) mwenye umri zaidi ya miaka 60 na ni mtoto 1 kati ya 5 (18%) mwenye umri chini ya miaka mitano ambao hupata huduma na matibabu bure katika vituo vya afya. Sera ya Nchi inasema kuwa huduma kwa wagonjwa wa nje kutoka makundi haya mawili ni bure, lakini wananchi wanasema kuwa wanatozwa pesa.
Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu? Wananchi na watumishi wa afya wazungumzia huduma za afya. Muhtasari huu ni kwa mujibu wa takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti kwa njia ya simu za mkononi, wenye uwakilishi wa kitaifa uliofanyika kwenye kaya zote Tanzania Bara.
Huduma za afya ni muhimu kwa kuwa zinahitajika sana na wananchi wengi. Zaidi ya nusu (57%) ya Watanzania waliotembelea vituo vya afya kati ya mwezi Mei na Juni 2013 walifanya hivyo kwa dhumuni la kutibiwa wao wenyewe au kumsindikiza mgonjwa. Watu walio wengi (77%) walitembelea zaidi vituo vya afya vya Serikali kuliko vya binafsi au vya dini. Hata hivyo, Watanzania wengi (63%) wanaamini kuwa Serikali inashughulikia vibaya suala la uboreshaji wa huduma za afya. Upatikanaji wa huduma za afya kwa kiasi kikubwa hutegemea uwepo wa watumishi wa afya na upatikanaji wa madawa. Mwezi Septemba 2013, Sauti za Wananchi iliripoti kuwa wagonjwa asilimia 41 hawakuweza kupata dawa kwenye vituo vya afya.
Endelea kusoma: afya
pakua nyaraka
- Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu? | Muhtasari |
833.19 KB
- Huduma na matibabu ya bure inavyowagharimu wazee na watoto | Taarifa kwa Vyombo vya Habari |
284.85 KB
- Do health facilities work for people? | Muhtasari |
433.84 KB
- Children and the elderly are paying the price for free treatment and care | Taarifa kwa Vyombo vya Habari |
288.4 KB
Tafsiri
unaweza pia kupenda...
- Tanzania: Afya Kwanza (30 Aug 2017)
- Kuongeza fedha pekee hakusaidii kumaliza tatizo la uhaba wa dawa (19 May 2014)
- Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu? (5 May 2014)
- Vijitabu vitano kuhusu vijana shujaa (17 Jan 2014)
- Gharama za kutibu Malaria (8 Oct 2013)
- Dawa zipo au zimekwisha? (19 Sep 2013)
- Dawa zipo au zimekwisha? (19 Sep 2013)