Twaweza.org

Machoni mwa umma: Maoni ya wananchi juu ya upatikanaji wa taarifa

Asilimia 84 ya wananchi wanaunga mkono kifungu cha sheria ya upatikanaji wa habari. Wananchi nane kati ya kumi wanaamini taarifa za mamlaka za umma zinapaswa kupatikana kwa wananchi wa kawaida (77%). Wengi wanaamini upatikanaji wa taarifa utasaidia kupunguza ama kuzuia rushwa na vitendo vingine viovu vinavyofanywa na viongozi wa umma (80%).

Haya ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Twaweza wenye jina, Jicho la Umma: Maoni ya wananchi kuhusu upatikanaji wa habari. Taarifa za utafiti huu zimekusanywa na Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika unaofanywa kwa njia ya simu za mkononi. Utafiti huu una uwakilishi wa nchi nzima. Matokeo ya utafiti huu yamejikita kwenye taarifa zilizokusanywa kutoka kwa wananchi 1,330 wa Tanzania Bara (Zanzibar haikushiriki katika utafiti) kati ya mwezi Machi na Aprili 2015.

Wananchi wanaunga mkono uwepo wa kifungu katika sheria ya upatikanaji wa habari ambacho kitatoa adhabu kwa viongozi wasiozingatia sheria. Aslimia 47 wameonyesha kifungu hicho ni cha muhimu kwenye sheria hiyo. Mwananchi mmoja kati ya watano (21%) anataka sheria hii izilazimishe mamlaka za umma kutoa taarifa. Pamoja na hayo, washiriki wametaka watoa habari walindwe (18%).

Endelea kusoma:

Authors: Angela Ambroz

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri