Twaweza.org

Tanzania kuelekea 2015: Maoni na matakwa ya wananchi juu ya uongozi wa kisiasa

Mwananchi mmoja kati ya watatu (33%) Tanzania Bara hajui ni nani atayekuwa chaguo lake la Rais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Hakuna mgombea hata mmoja anayependwa na wapiga kura kwa zaidi ya 15%. Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Twaweza mwezi Septemba 2014, anayeongoza ni Edward Lowassa (13%) akifuatiwa na Mizengo Pinda (12%) wote wa CCM, na watatu ni Dkt. Wilbrod Slaa wa Chadema (11%). Wafuasi wa CCM walipohojiwa, robo yao (24%) walisema watampigia kura yeyote atakayeteuliwa na chama.

Ukilinganisha kukubalika kwa vyama, nusu ya Watanzania (54%) wamesema wataipigia kura CCM kwenye uchaguzi wa Rais, na robo moja ya Watanzania (23%) wataipigia kura CHADEMA. Walipoulizwa watafanya nini kama vyama vya upinzani vitaungana na kusimika mgombea mmoja tu, kama UKAWA ilivyoahidi kufanya, CCM bado inaongoza lakini idadi ya watakaoichagua CCM inapungua hadi chini ya nusu (47%) ya wananchi wote. Wakati huohuo, karibu wananchi watatu kati ya kumi (28%) wamesema wangempigia kura mgombea wa upinzani. Idadi kubwa ya wananchi, mmoja kati ya watano (19%) amesema hatapigia kura chama bali mgombea. Ikitokea kundi hili likaamua kumpigia kura mgombea wa upinzani, ushindani utakuwa mkali mwaka 2015.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Tanzania kuelekea 2015: Maoni na matakwa ya wananchi juu ya uongozi wa kisiasa. Muhtasari huu umetokana na Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu ya mkononi maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haimo kwenye matokeo haya). Matokeo muhimu yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,445 mwezi Septemba 2014.

Kukagua takwimu

Endelea kusoma:

Authors: Elvis Mushi

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri