Twaweza.org

Kusimamia Maliasili: wananchi wanasemaje?

Wananchi wanne kati ya watano wanaamini kuwa mafuta na gesi yatawanufaisha wao, watoto wao na nchi yao kwa ujumla. Wakati huo huo, wananchi wanne kati ya kumi (37%) wanaamini kuwa viongozi wa Serikali na matajiri ndio wataofaidika zaidi. Pia, zaidi ya nusu (55%)  wangependa baadhi ya mapato ya mafuta na gesi wapewe wananchi moja kwa moja kama fedha taslimu.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Kusimamia Maliasili: Wananchi wanasemaje? Utafiti huu ulifanywa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu ya mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa.

Utafiti unaonesha kwamba matakwa ya wananchi ni kuwa, angalau kiasi cha mapato ya mafuta na gesi kipelekwe moja kwa moja kwa wananchi. Mwananchi mmoja kati ya watano (20%) angependelea kiasi kikubwa cha fedha kipelekwa moja kwa moja kwa wananchi; wakati wananchi asilimia 18 wangependelea kuwe na mgawo sawa wa mapato kati ya serikali na wananchi. Asilimia 17 wangependelea Serikali ipate asilimia kubwa zaidi ya mapato kwa ajili ya kuendeleza miundombinu na huduma za kijamii na wananchi wapewe kiasi kinachobaki.

Hata hivyo, Watanzania walio wengi (43%)  wangependa mapato yote yaende Serikalini kwa ajili ya kugharamia huduma muhimu. Isitoshe, wananchi walipoulizwa namna wanavyoamini mapato ya rasilimali yanaweza kuleta manufaa kwa Watanzania, nusu yao (46%) walisema mapato yatumike katika kutoa huduma za afya na elimu, na wananchi wanne kati ya kumi (20%) walipendekeza yatumike kwenye miundombinu au kwenye mipango ya kupambana na umaskini (17 %).
 

Endelea kusoma:

Authors: Mtemi Zombwe

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri