Twaweza.org

Masuala ya Muungano: Maoni ya wananchi kuhusu kinachoendelea Zanzibar

Zanzibar ilikumbwa na matukio mengi wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015. Matokeo ya uchaguzi yalifutwa baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kusema “kulikuwa na ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi.” Uchaguzi mpya ulipangwa kufanyika mwezi Machi 2016.  Maamuzi hayo yalipingwa vikali na upinzani na kutiliwa shaka na miongoni mwa wajumbe wa jumuia ya kimataifa. Viongozi wa upinzani pamoja na wafuasi wao waligoma kushiriki kwenye uchaguzi mpya. Matokeo yake mgombea wa Chama Cha Mapinduzi aliyekuwa madarakani Rais Ali Mohamed Shein akaibuka na ushindi kiurahisi.

Pamoja na matukio hayo, nusu ya wananchi wa Tanzania Bara (53%) wanasema hawafahamu kile kilichojiri Zanzibar tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa Oktoba. Wananchi 4 kati ya 10 wana taarifa kuwa uchaguzi mpya ulifanyika tarehe 20 Machi 2016 (43%) na wanafahamu kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba yalifutwa (39%).

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kupitia muhtasari wa utafiti wake wenye kichwa cha habari, “Masuala ya Muungano: Maoni ya wananchi kuhusu kinachoendelea Zanzibar”. Muhtasari huo unatokana na takwimu zilizokusanywa na Sauti za Wananchi, Utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa na unaotumia simu za mkononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,815 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 29 Machi na tarehe 12 Aprili 2016.
 

Endelea kusoma:

Authors: John Mugo

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri