Twaweza.org

Vijana wenye kipaji cha zana za teknolojia waweka takwimu za elimu wazi

Mkutano wa Ushirika wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) umezinduliwa rasmi jijini London, Uingereza, na mwaliko wa kuhudhiria katika mkutano huu umemfikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete. Umoja wa vijana nchini wakitumia fursa ya mkutano huu, wakiwa wataalamu wa zana za teknolojia, wamezindua wavuti uitwao shule.info ili kuonyesha umuhimu wa takwimu zilizo wazi. Wavuti hii unakusanya takwimu za matokeo ya mitihani ya Kidato cha 4 kuanzia mwaka 2004 na kuzipanga katika namna ambayo ina urahisi wa kusoma na wepesi wa kueleweka.

Inatarajiwa kuwa wavuti hii itakuwa wa muhimu sana kwa wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi na watunga sera, ambao wote kwa pamoja wataweza kupata takwimu wanazozihitaji kwa urahisi. Watunga sera wataweza kuzitumia takwimu za shule moja moja na mikoa na kutazama wapi kumekuwa na mafanikio na wapi pameanguka, wakati wazazi wataweza kulinganisha shule na kufanya uamuzi kutokana na taarifa hizo kuwa wawapeleke watoto wao katika shule zipi. Wanafunzi  nao watafanikiwa kupata kadi zao za matokeo kwa kuingiza namba zao za utahiniwa na vituo vya mitihani. Majina ya watahiniwa hayajawekwa katika tovuti hii bali mwanafunzi atatambulika kwa namba yake ya utahiniwa.

Wavuti inapatikana kupitia www.shule.info

Shule.info ni wavuti iliyo hai ambapo kwa sasa inapatikana kupitia program ya majaribio ya Beta. Maoni kuhusu wavuti hii yanakaribishwa kutoka kwa watu wote, hasa wanahabari kupitia anwani hii matokeo.shuleni@gmail.com

Wavuti umeandaliwa na Arnold Minde na timu ya waendelezaji zana za teknolojia Watanzania, wakifadhiliwa na Twaweza.

Endelea kusoma: elimu

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri