Twaweza.org

Safi na Salama? Maji na Usafi wa Mazingira

Inaonekana kwamba hakuna mabadiliko makubwa yaliyotokea katika upatikanaji wa maji nchini Tanzania, hususani katika maeneo ya vijijini, katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Ingawa kuna taarifa nyingi zenye takwimu juu ya hali ya maji nchini, ni taaarifambili tu zinashabihiana na kuonesha uwepo wa maboresho katika upatikanaji wa maji ndani ya miaka ya karibuni.

  • Utafiti wa Sauti za Wananchi umeonesha ya kwamba Upatikanaji wa maji vijijini ulikuwa asilimia 55 mwaka 2014 na asilimia 46 mwaka 2016 – Ofisi ya Taifa ya takwimu inaonyesha tofauti ya upatikanaji wa maji kuwa kati ya asilimia 40 na 50 kwa zaidi ya miaka 10 ambapo tafiti tisa kati ya kumi zimeonesha uwiano wa takwimu ndani ya kiwango hiki.
  • Wizara ya Maji  nayo imeripoti upatikanaji mkubwa wa maji wa kati ya asilimia 50 na 60 ndani ya kipindi tajwa.
  • Takwimu za Matokeo Makubwa Sasa zinaripoti kuongezeka kwa kasi ya upatikanaji wa maji kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi asilimia 67 mwaka 2015.

Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika utafiti unaoitwa Safi na Salama? Maji, usafi na Afya Mazingira. Muhtasari huu unatokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia njia ya simu. Takwimu hizi zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,808 wa Tanzania Bara mnamo mwezi Oktoba mwaka 2016 (Zanzibar haikuhusishwa katika utafiti huu).

Utafiti umeonesha kuwa, zaidi ya nusu ya wananchi (asilimia 54) wameripoti kutumia vyanzo vya maji vilivyoboreshwa katika kujipatia maji ya kunywa. Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya kaya za mijini (asilimia 74) na vijijini (asilimia 46) na kati ya makundi ya  matajiri (asilimia 75) na masikini (asilimia 41) kwenye utumiaji wa vyanzo vilivyoboreshwa.
Katika maeneo ya vijijini, vyanzo vinavyotumiwa zaidi ni visivyoboreshwa kama vile visima visivyojengewa uzio (asilimia 26) na maji ya ardhini (asilimia 20). Vyanzo hivi havijaboreshwa. Kaya chache sana zinatumia vyanzo vilivyoboreshwa kwa mfano mabomba ya umma (asilimia 17), au visima vilivyojengewa (asilimia 16).
 

Endelea kusoma: maji

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri