Twaweza.org

TEDxDar na mikinzamo ya maendeleo

TEDxDar, iliyoandaliwa na kundi la vijana wa Kitanzania mwishoni mwa mwezi Mei, ni tukio la kujitegemea limelozaliwa na TED, “jamii” ya kimataifa iliyojikusanya kinamna fulani ikiunganishwa na “fikra zinazostahili kusambazwa kwa teknolojia, burudani na sanaa au ubunifu”. Tukio hili liliweza kuwakutanisha wavumbuzi wa kusisimua ndani ya Tanzania. Kiongozi wa Twaweza, Rakesh Rajani, alizungumzia wapi vuguvugu la mabadiliko linapoanzia, akiibua mifano toka katika uzoefu wake wakati wa uchambuzi yakinifu (wa kitafiti) wa hali ilivyo wakati wa uundwaji wa Twaweza, pamoja na ziara ya mafunzo vijijini iliyofanywa na wafanyakazi wa Twaweza mwaka 2009. Ziara hii imekua ikijadiliwa kwa mapana katika majukwaa ya blogu mbalimbali kwa wiki kadhaa zilizopita, zikipeperushwana  Owen Barder, Swahili Street, Elsie Eyakuze na wengineo. Unaweza kufatilia haya majadiliano na pia soma kuhusu uzoefu wa Twaweza katika vijiji tisa ndani ya Tanzania.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri