Twaweza.org

Ushirikiano wa Serikali-Wazi wazinduliwa

Mkakati mpya wenye malengo makubwa ya dunia nzima uitwao, Open Government Partnership (OGP) umezinduliwa Washington DC tarehe 12 Julai, 2011. OGP ni mpango wa ulimwengu kuboresha utendaji wa serikali. Sote tunahitaji serikali zilizo wazi zaidi, fanisi na zinazowajibikazenye taasisi zinazowajenga uwezo raia na kusikiliza matakwa yao.

Mkakati wa serikali-wazi unalenga kupata serikali zilizonuia kuboresha uwazi, kujenga uwezo wa raia, kupambana na rushwa na kutumia teknolojia mpya kuimarisha utawala. Ili kuweka msisitizo wa ushiriki wa wadau wengi mbalimbali, OGP inasimamiwa na kamati tendaji inayojumisha watu toka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali. Twaweza ni mojawapo ya wanachama wa kamati tendaji, na imeshirikishwa katika kuunda wazo la OGP tangu mwanzoni.

Serikali hamsini na tisa na ASIZE 80 zimeshiriki katika uzinduzi. Kenya na Uganda zilikuwa wawakilishi katika ngazi ya juu. Tunatarajia Tanzania pia itajiunga hivi karibuni.

Kwa taarifa zaidi, tembelea, Open Government Partnership. Kujua namna gani nchi zinaweza kushiriki kwenye mchakato huu, chukua OGP’s Roadmap to Participation. Waweza angalia uzinduzi rasmi hapa.

Endelea kusoma: kutumia teknolojia

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri