Twaweza.org

Utapiamlo umeua watoto 600,000 kwa muongo mmoja

Daily News, gazeti la Kiswahili la Tanzania, linaandika kuwa mlo usiokidhi umegharimu maisha ya zaidi ya watoto 600,000 walio chini ya umri wa miaka mitano katika muongo uliopita. Likinukuu muhtasari wa utafiti wa Twaweza, Daily News linaeleza kuwa mlo hafifu ni mzigo kiuchumi kwani TZS 650bn/- zinatumika kila mwaka kutibu magonjwa ambayo yanaepukika kwa kula mlo sahihi.

Habari hii pia inaonesha juhudi zinazoendelea kuweka taratibu, sheria na viwango vya uhamilishaji wa vyakula vikuu. Muhtasari wa utafiti unaonesha kuwa mwaka 2010 pekee watoto 43,000 walikuwa katika hatari ya kufa kutokana na utapiamlo mkali. Habari kamili hapa. Fungua muhtasari wa sera hapa.

Endelea kusoma: afya Daily News

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri