Twaweza.org

Uwazi

Twaweza imeanzisha kitengo cha Uwazi ambacho kinawapa wabia wa Twaweza, vyombo vya habari na mawakala wakuu wa mabadiliko (wabunge, waandishi wa habari, wakuu wa serikali) taarifa zilizojengwa juu ya msingi wa takwimu, na zinazowasilisha ujumbe ulio wazi na unaoeleweka kirahisi.

Uwazi inatafiti teknolojia mpya za kukusanya na kuwasilisha takwimu (tafiti kupitia simu za mkononi mifumo ya IVR, ushahidi, kubuni na kuanzisha huduma mbali mbali). Hizi ni pamoja na Wananchi Survey, itakayoanzishwa hivi karibuni, ambayo itakuwa ni njia ya kisayansi ya kupata maoni ya jamii na hali halisi kila wiki, pamoja na mfululizo wa machapisho ya taarifa mbali mbali. Makao makuu ya Uwazi yatakuwa Dar es Salaam, lakini kutakuwa na wafanyakazi na pia kufanya kazi kwa ushirikiano na vitengo vya utafiti nchini Kenya na Uganda.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri