Twaweza.org

Uwezo Kenya kuzindua ripoti ya upimaji ya mwaka 2011

Taasisi ya wanawake watafiti wa elimu Kenya imetangaza kuwa mnamo Julai 19 mwaka huu itazindua ripoti ya upimaji wa Uwezo kitaifa ya mwaka 2011. Wakati uzinduzi wa ripoti hiyo ukifanyika kitaifa kwenye viwanja vya Taasisi ya Elimu ya Kenya (KIE) kutakuwa pia na matukio ya uzinduzi kwenye mikoa ifuatayo: Magharibi, Bonde la Ufa, Mashariki, Kaskazini Mashariki na Eldoret. Lengo la maadhimisho ya kimkoa ni kuwahusisha wadau wengi zaidi wa elimu wakati wa kutoa matokeo ya utafiti na hivyo kuwahamasisha raia kuchukua hatua kuboresha kiwango cha elimu inayotolewa mashuleni.

Njoo mara nyingine kwenye tovuti hii usome habari zaidi za uzinduzi huo.

Endelea kusoma: kenyan primary education

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri